Nitafanya kila kitu Sailors Gang irudi kwa game - Miracle Baby

Muhtasari

• Msanii wa kundi la Sailors, Peter (Miracle Baby) amesema kwamba anafanya kila awezalo kuhakikisha wanarejea kwenye muziki.

• Msanii wa kundi la Sailors, Peter (Miracle Baby) amesema kwamba anafanya kila awezalo kuhakikisha wanarejea kwenye muziki.

• Kwa sasa mashabiki ambao wameonekana kuwa na Imani kwao wanasubiri kwa hamu urejeo wa mabingwa hao ili wazidi kufurahisha masikio na macho yao kupitia muziki mzuri

Sailors-3-551x600
Sailors-3-551x600
Image: Hisani

Msanii wa kundi la Sailors, Peter (Miracle Baby) amesema kwamba anafanya kila awezalo kuhakikisha wanarejea kwenye muziki.

Kupitia ujumbe wake ulioambatanishwa na picha ya kundi hilo katika mtandao wa Instagram, Miracle Baby ambaye ni mtangazaji wa kipindi katika kituo kimoja cha runinga hapa nchini, amesema kwamba Mungu ana kila sababu ya wao kupotea kwenye muziki na anaamini kwamba watarudi wakiwa na nguvu zaidi ili kuzidi kuwaburudisha mashabiki wao.

Aidha amekiri kwamba wasanii hao wamekua naye tangu utotoni hivyo basi watasalia kuwa marafiki zake wa kweli  licha ya kukejeliwa na kusisitiza kwamba kuna siku nyota yao itang'aa tena.

"Ata kwende aje, hii ndo rende natambua toka utotoni Soo ata tuchekwe I swear ninatry my best kuwarudisha game soon kueni strong God ako na reason zake," alisema Miracle Baby.

Kundi hilo lilihusisha wasanii wanne wakiwemo: Peter ( Miracle Baby), Shalkido (African Boy), Alexander Ikuru Wanjiku (Lexy Young) na Qoqosnuma.

Hili linajiri baada ya wasanii hao kuzama kwa muda mrefu sasa huku mashabiki wakijiuliza maswali kuhusu ni kipi kilichozima nyota yao katika burudani la Kenya, ambapo vijana hawa waliteka nyoyo za mashabiki hao kupitia nyimbo zao zenye mtindo was Gengetone.

Vijana hawa walikuja kutambulika zaidi mnamo mwaka wa 2019 kupitia ngoma yao ya #Wamlambez ambayo alitinga views milioni tano katika mtandao wa YouTube.

Aidha ngoma hiyo iliondolewa mtandaoni kwa amri ya aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Kenya Film and Classification Board (KFCB) Ezekiel Mutua, kwa kile alichokitaja Kama ngoma hiyo kukosa maadili katika jamii.

Ikumbukwe kwamba kundi hili lilianza kupoteza nyota yake mwaka wa 2020 baada ya Mwalimu Rachel kusitisha huduma zake na zile za kampuni yake ya MRX katika kusimamia kundi hilo, akisema kwamba alifanikiwa kufanya shughuli kubwa ya kuhakikisha Wakenya wanatambua vipaji hivyo.

Kwa sasa mashabiki ambao wameonekana kuwa na Imani kwao wanasubiri kwa hamu urejeo wa mabingwa hao ili wazidi kufurahisha masikio na macho yao kupitia muziki mzuri.