Aristote alemewa, aifuta akaunti yake ya Instagram

Muhtasari

• Mfanyibiashara kutoka Tanzania, Aristote amelazimika kufuta akaunti yake ya Instagram baada ya bifu yake na Wema Sepetu kuzidi maji.

•Hili linajiri baada ya mashabiki wake Wema Sepetu na baadhi ya viongozi kumkashifu vikali kutokana na kitendo chake cha kumkejeli muigizaji huyo kuhusu hali yake ya maisha.

Irene Uwoya
Irene Uwoya
Image: Instagram KWA HISANI

Mfanyibiashara kutoka Tanzania, Aristote amelazimika kufuta akaunti yake ya Instagram baada ya bifu yake na Wema Sepetu kuzidi maji.

Hili linajiri baada ya mashabiki wake Wema Sepetu na baadhi ya viongozi kumkashifu vikali kutokana na kitendo chake cha kumkejeli muigizaji huyo kuhusu hali yake ya maisha.

Inakisiwa kwamba Aristote alikosa kustahimili uzito wa matusi na presha kutoka kwa mashabiki na hivyo kulazima kutoka Instagram ili kupata utulivu wa kiakili wakati huu kila shabiki anamuona kuwa mtu asiyekuwa na heshima kwa binadamu wengine.

Ikumbukwe kwamba Aristote Jumatatu 31/01/2022 aliachia video akiomba msamaha kwake Wema Sepetu akisema kwamba hakukusudia ishu hiyo kufikia kiwango hicho, hapo Sepetu hajaweza kujibu msamaha huo.

Kwa sasa inasubiriwa kuona iwapo mwanabiashara huyo atarejea tena kwenye Instagram na kutoa taarifa kamili kuhusu kusepa kwake.