Sio haki kabisa, msituongezee bei za bidhaa - Huddah Monroe

Muhtasari

• Mwanamitindo na mwanabiashara, Huddah Monroe ameshtumu wachuuzi kwa kile anachokidai kama kuwauzia watu maarufu bidhaa kwa bei iliyozidishwa.

• Kulingana na ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Huddah amekiri kwamba ukiwa mtu maarufu na ununue bidhaa yoyote, muuzaji anahakikisha umelipa mara tatu zaidi ya bei anayolipa mtu wa kawaida.

Image: INSTAGRAM// HUDDAH MONROE

Mwanamitindo na mwanabiashara, Huddah Monroe ameshtumu wachuuzi kwa kile anachokidai kama kuwauzia watu maarufu bidhaa kwa bei iliyozidishwa.

Kulingana na ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Huddah amekiri kwamba ukiwa mtu maarufu na ununue bidhaa yoyote, muuzaji anahakikisha umelipa mara tatu zaidi ya bei anayolipa mtu wa kawaida.

“wanachukulia kuwa watu maarufu sio watu wa kawaida,anaweza kumtafuta mtu kwa ajili ya biashara ila akijua ni mtu maarufu tu basi bei itapanda hata mara 3 lakini akitumiwa mtu wa kawaida atafanyiwa bei ya kawaida,” aliandika Huddah.

Huddahthebosschick
Huddahthebosschick
Image: Instagram KWA HISANI

Amewarai wafanyibiashara wote kuelewa kwamba mastaa ni binadamu pia na hivyo wanapaswa kuuziwa kama wengine.