Eddie Butita asiponiomba msamaha nitamtafuta nimvuruge - Vincent Mboya

• Mwanablogu Vincent Mboya amedokeza kwamba Eddie Butita alimtupa nje ya sehemu kulikokuwa kunafanyika hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mcheshi Comedian YY.

• Akizungumza na vyombo vya habari, Mboya amesema kwamba alikuwa amekwenda kushuhudia sherehe hiyo kwa kuwa tangazo lilisema kuwa kila mtu alikuwa amealikwa kwenye sherehe hiyo iliyofanyika katika klabu moja jijini Nairobi.

Vincent Mboya
Vincent Mboya
Image: Instagram KWA HISANI

Mwanablogu Vincent Mboya amedokeza kwamba Eddie Butita alimtupa nje ya sehemu kulikokuwa kunafanyika hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mcheshi Comedian YY.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mboya amesema kwamba alikuwa amekwenda kushuhudia sherehe hiyo kwa kuwa tangazo lilisema kuwa kila mtu alikuwa amealikwa kwenye sherehe hiyo iliyofanyika katika klabu moja jijini Nairobi.

 Kulingana na Mboya, tukio hilo lilitokea baada yake kumwambia Butita kwamba hajui kuvaa nguo nzuri jambo ambalo liliibua chuki kati yao wawili.

Aidha, ameongeza kuwa anahitaji ulinzi mkali kwa kuwa maisha yake yapo hatarini na kwamba anapokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wasanii humu nchini.

Ameongeza kwamba licha ya vurugu iliyoshuhudiwa hatopeleka kesi hiyo katika kituo cha polisi, na pia amempa Butita siku kumi nan ne amtafute na kuomba msamaha la sivyo atamtafuta na kumfanyia yaleyale aliyomfanyia katika sherehe hiyo.

Mboya amesema kwamba ataendelea kuwakosoa wasanii ambao wanafanya mambo ndivyo sivyo humu nchini.

Vincent Mboya
Vincent Mboya
Image: Instagram KWA HISANI