Nilimblock Willy Paul lakini bado ananitafuta - Miss P

Muhtasari

• Miss P amesema kwamba alimbock aliyekuwa bosi wake Willy Paul kila mahali na kumsahau

• Alisema kwamba ako na uhakika kwamba Paul amejaribu kumtafuta mara kadha lakini yeye alishamblock kila mahali.

Miss P
Image: INSTAGRAM

Msanii Miss P amesema kwamba aliyekuwa bosi wake wa kimuziki Willy Paul bado anaendelea kumfuatilia kichinichini licha ya yeye kumblock kila mahali mpaka kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na mtangazaji Ankali Ray, Miss P alisema kwamba hataki kumsikia tena msanii huyo kwani alishamsahau na mpaka kumfananisha na kusahau mtu aliyekufa na kusahaulika.

Alipoulizwa lini mara ya mwisho aliongea na Willy Paul, Miss P alisema kwamba hata hakumbuki mara ya mwisho kuzungumza na yeye na kusema kwamba alishamchunia nje na kumsahau kikweli.

Alisema kwamba ako na uhakika kwamba Paul amejaribu kumtafuta mara kadha lakini yeye alishamblock kila mahali.

Miss P na Willy Paul
Image: INSTAGRAM

“Siwezi hata kumbuka mara ya mwisho niliongea na yeye. Mimi hata sijawahi mkumbuka na nilishamsahau. Ukishamzika mtu kwenye akili yako, ushamsahau kabisa,” alisema Miss P

Ray alipomuulizia kuhusu Sakata zima la kesi mahakamani, Miss P alisema alimuachia wakili wake kila kitu na hata hajui maendeleo ya kesi hiyo na pia amefichua kwamba chenye kilitokea kilishatokea na hawezi rudisha maneno yake kwa sababu Willy Paul ndiye alianza kuchukua mkondo wa mahakamani.

Baada ya kutengana na rekodi lebo ya Saldido International yake Willy Paul, Miss P alitoka na baadae kuzua masuala ya bosi wake kumdhulumu kingono na baadae akatangaza kufanya kazi na kampuni ya mchekeshaji Eric Omondi.

Siku za hivi karibuni baada ya wafuasi wake kukisikia kimya chake chenye sauti, walidadisi uwepo wake na Omondi akaibuka na madai kwamba Miss P si msanii anayependa kujituma na hivyo wamefikia uamuzi wa kukatisha mkataba wao na msanii huyo.

Sasa suali kubwa ni je, ni nini cha ziada kwa msanii Miss P na safari yake ya muziki nchini Kenya?