Msanii Vivianne vitani na Ngomma

Muhtasari

• Msanii Vivianne ameteta mitandaoni kuhusu mkurugenzi mktendaji wa Ngomma VAS kufanya udanganyifu kwenye miziki ya wasanii.

• Msanii huyo anasema kwamba kwa sasa bado yuko mgonjwa na anataka kampuni ya Ngomma imuachie haki zote za kusimamia kazi zake za kimuziki.

Vivianne Kenya
Image: Facebook

Msanii maarufu nchini Vivianne amezua madai makali kwenye ukurasa wake wa Instagam huku akimtuhumu mkurugenzi mtendaji wa kampuni inayosukuma muziki Afrika, Ngomma VAS kwa ufisadi katika miziki ya wasanii wa Afrika.

Msanii huyo anasema kwamba kwa sasa bado yuko mgonjwa na anataka kampuni ya Ngomma imuachie haki zote za kusimamia kazi zake za kimuziki.

Vivianne amemtuhumu mkurugenzi mtendaji wa Ngomma kuacha kudanganya kwa kile ambacho hakuwekeza.

Image: Instagram

“Nimekatishwa tamaa sana na Ngomma. Nina heshima iliyotukuka kwa mkurugrnzi mtendaji. Acha kudanganya kwa kitu ambacho haukuwekeza, tatizo lako nig ani? Tulikusaidia kujenga kampuni yako. Niachieni mimi na wenzangu tutoke kwa amani,” Vivianne alilalama.

Vivianne ameendelea kuteta kwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo na kusema kwamba hakuja haja yake yeye kuzishikilia kazi zake kwa sababu anafaa kujua kando na usanii, yeye pia ni mfanyibiashara.

Vivianne amesema kwamba lengo lako kuu ni kuachiwa haki zote za kusimamia kazi zake zote ambazo amezitunga.

“Siku zote nimekuwa mnyenyekevu na mwenye heshima sana lakini sasa nataka kila wimbo ambao mpenzi wangu na mimi tumefanya ziwe chini ya uongozi wangu,” Vivianne ameandika.