Fanyeni kazi wasanii, msipende kiki - Octopizzo

Muhtasari

• Msanii Octopizzo ameonyesha kukasirishwa kwake kwa wanamuziki na wasanii wote ambao wanajihusisha katika masuala ya kutengeneza kiki.

• Octopizzo ni moja kati ya rapa ambao hawajihusishi na vurugu nyingi kwenye gemu la burudani, jambo ambalo limemfanya kudumu kwenye muziki kwa muda mrefu.

Octopizzo
Octopizzo
Image: Instagram KWA HISANI

Rapa matata Octopizzo ameonyesha kukasirishwa kwake kwa wanamuziki na wasanii wote ambao wanajihusisha katika masuala ya kutengeneza kiki.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Pizzo amewauliza wasanii iwapo wanafanya kiki ili kujikuza kikazi au kutafuta umaarufu.

“Mnaotafuta kiki, wasanii na wanamuziki, je mnafanya hivo kukuza vipaji vyenu ama kupata umaarufu?” Aliuliza Octopizzo.

Katika siku za hivi karibuni wanamuziki wengine wameonekana kufanya kiki ili kusukuma kazi zao, jambo ambalo msanii Octopizzo hajalipokea kwa furaha.

Kulingana naye, angependelea wasanii kutia bidii katika kutoa nyimbo nzuri ambazo zitapokelewa na mashabiki bila ugumu wowote utakaolazimu wao kutoa kiki.

Octopizzo ni moja kati ya rapa ambao hawajihusishi na vurugu nyingi kwenye gemu la burudani, jambo ambalo limemfanya kudumu kwenye muziki kwa muda mrefu.