Siwezi kaa zaidi ya saa 3 mbali na mwanangu - Vera Sidika

Muhtasari

• Vera Sidika amesema kwamba hawezi zidisha muda wa saa tatu akiwa mbali na mwanae kwani hatohisi mwenye amani kabisa nafsini mwake.

• Vera alisema kwamba ana vigezo vingi tu vya kumchagua mlezi wa mwanae na akasema kwamba kigezo kikuu ni mtu asiyekuwa na uraibu wa mitandaoni na mwenye umri wa miaka 40 kwenda mbele

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti Vera Sidika ameelezea kwamba hawezi akakaa mbali na mwanawe kwa muda aidha kwa shughuli za kikazi ama za kibinafsi.

Sidika amesema kwamba hawezi zidisha muda wa saa tatu akiwa mbali na mwanawe kwani hatohisi mwenye amani kabisa nafsini mwake.

Akiandika kwenye Instagram yake, Sidika amesema kwamba anampenda sana mwanawe Asia na kufichua kwamba hata hajawahi ona vibaya akimlilia usiku kwa njaa na kubadilishwa diapers za watoto kwani anajihisi mwenye furaha kufanya hivo.

“Mwanangu ni wa thamani kubwa na nampenda sana. Hakuna kitu ambacho kimewahi niudhi ama kunifanya nijihisi kuchoka. Uso wake ni mzuri sana wa kuangaliwa kila mara,” aliandika Vera.

Mwanasosholaiti huyo ambaye pia ni mfanyibiashara aliongeza kwamba hata kama yuko na shughuli na nyingi za hapa na pale, mara nyingi mwanawe ndiye huchukua nafasi ya kwanza katika shughuli zake hizo na kusema kwamba anazunguka na mlezi kila mahali ili kuhakikisha yuko karibu na Asia.

Vera alisema kwamba ana vigezo vingi tu vya kumchagua mlezi wa mwanawe na akasema kwamba kigezo kikuu ni mtu asiyekuwa na uraibu wa mitandaoni au hata mwenye asiyejishughulisha na mitandao kabisa na ambaye lazima awe na umri wa miaka 40 kwenda mbele.

Katika instastories zake, Vera alisema kwamba muda mwingi kabisa ambao atakuwa mbali na mwanawe ni saa tatu, huku saa ya mwisho ikiwa ni ya kusafiri kutoka maeneo ya kazi kuelekea nyumbani kwake.