"Maneno hayawezi kueleza upendo wangu kwenu" Vera asherehekea mumewe na bintiye kwa ujumbe maalum

Muhtasari

•Vera amemtaja mumewe kama baba bora zaidi duniani kwa binti yao na mume  ambaye hawezi kulinganishwa na wanaume wengine.

•Mauzo amemshukuru sana Vera kwa kumchagua kama mume wake huku akimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti mashuhuri nchini Vera Sidika ametumia siku ya Valentines kusherehekea familia yake ndogo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amehakikishia mumewe Brown Mauzo na binti  yao Asia Brown kwamba upendo  wake kwao ni zaidi ya maneno tu.

Mwanasoshalaiti huyo amesema Valentines ya mwaka huu ni maalum sana kwake kwa kuwa anapata kuisherehekea na mumewe pamoja na mtoto wao.

"Siku hii ya wapendanao ni ya pekee zaidi kwa sababu ninapata kuisherehekea pamoja na mtoto wangu Asia na mwanamume mzuri zaidi kuwahi kutembea duniani na anayejali Brown Mauzo maneno hayawezi kuelezea upendo wangu kwako na kwa familia yetu ndogo ya kupendeza." Vera  alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja alimtaja mumewe kama baba bora zaidi duniani kwa binti yao na mume  ambaye hawezi kulinganishwa na wanaume wengine.

Vera amefufua kumbukumbu kwamba bintiye alitungwa tumboni mwake mnamo siku kama hii ya Valentines mwaka uliopita. 

Umekuwa baba bora zaidi kwa binti yetu na uthibitisho kwamba wanaume wazuri bado wapo. Heri za siku ya wapendanao kwa mapigo ya wapenzi wangu Brown Mauzo na Asia Brown. Nawapenda nyote.Kwa kweli, mwaka jana siku kama hii Asia alikuwa akiogelea kuelekea tumboni mwangu" Vera amesema.

Mauzo kwa upande wake amesema kwamba amefanya siku ya Valentines maalum kwa familia mkewe Vera.

Mwanamuziki huyo amemshukuru sana Vera kwa kumchagua kama mume wake huku akimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.