Kakake Vera azungumzia fununu za ndoa na Mauzo

Muhtasari

• Kinger Josh ambaye ni kaka yake Mwanasosholaiti Vera Sidika amezungumzia madai kuhusu harusi baina ya dadake na shemejiye Brown Mauzo

• Kakake na Vera aidha alimsifia shimeji wake Mauzo kwa kumtaja kuwa mtu mzuri na mwenye mapenzi ya dhati kwa dadake Vera.

Image: HISANI

Kinger Josh ambaye ni kaka yake Mwanasosholaiti Vera Sidika amezungumzia madai kuhusu harusi baina ya dadake na shemejiye Brown Mauzo, kama ambavyo mwanamuziki huyo alivyodokeza wiki chache zilizopita.

Katika mahojiano ya kipekee na Mpasho, Josh alipatwa na kigugumizi baada ya kuulizwa kuhusu fununu za kufanyika kwa ndoa hiyo na kama familia yao ilihudhuria.

“Siwezi zungumzia suala hilo la ndoa,” alisema Josh

Kwa kujibu iwapo familia yake ilijumuishwa katika harusi yenyewe kama ilifanyika, Kinger Josh alikwepa na kumwambia mwanahabari wa Mpasho kwamba ni vizuri amuamini kwa yale machache ambayo atayasema kwani hawezi kuzungumzia suala la ndoa hiyo kwa kina.

“Dadangu alisema wameoana na sisi kama familia tuliitikia na maneno yake hayo kwa sababu ni mahusiano yao,” alisema Josh

Kakake na Vera aidha alimsifia shimeji wake Mauzo kwa kumtaja kuwa mtu mzuri na mwenye mapenzi ya dhati kwa dadake Vera.

Vera alizua gumzo mitandaoni mwaka wa 2020 baada ya kuandika kwenye kurasa zake kwamba hayupo tena sokoni kwani ashapata mwenza na mpaka kumtaja Mauzo kuwa mlengwa.

Wengi hawakuamini kwani hakupakia picha zao wakiwa Pamoja ila ilikuja kubainika kuwa kweli baadae mwaka 2021 na ambapo walitangaza kuwa na ujauzito na kufanikiwa na mtoto kwa jina Asia.