Vera amjibu shabiki aliyesema mtoto wake anafanana na Otile

Muhtasari

• Katika ukurasa wake wa Instagram, Sidika huwa anaruhusu watu kumuuliza maswali mara kwa mara kwa kile kinachojulikana kama Q&A na hujikaza kujibu kadri ya uwezo wake.

• Hivi karibuni amemjibu shabiki mmoja aliyeandika maoni akisema kwamba mtoto Asia anafanana na aliyekuwa mpenzi wake Otile Brown, jambo ambalo Vera alijibu kwa kicheko na mshangao.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Tofauti na mastaa wengine wasiojishughilisha na maoni ambayo mashabiki wao huandika kwenye vitu ambavyo wasanii hao hupakia kwenye mitandao, Vera Sidika ni kama yeye huyapitia sana maoni mbali mbali ya mashabiki kwenye kurasa zake mitandaoni.

Hili linadhihirika wazi ambapo katika siku za hivi karibuni amekuwa akiyajibu maoni hayo kutoka kwa mashabiki mbali mbali wanaotaka kujua vitu tofauti tofauti katka maisha yake na haswa kuhusiana na mtoto wake Asia pamoja na mapenzi yake na msanii Brown Mauzo.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Sidika huwa anaruhusu watu kumuuliza maswali mara kwa mara kwa kile kinachojulikana kama Q&A na hujikaza kujibu kadri ya uwezo wake.

Hivi karibuni amemjibu shabiki mmoja aliyeandika maoni akisema kwamba mtoto Asia anafanana na aliyekuwa mpenzi wake Otile Brown, jambo ambalo Vera alijibu kwa kicheko na mshangao.

Baada ya kujibu swali hilo ambalo anaonekana hakulitarajia kutoka kwa mashabiki wake, Hivi karibuni amemjibu shabiki mmoja aliyeandika maoni akisema kwamba mtoto Asia anafanana na aliyekuwa mpenzi wake Otile Brown, jambo ambalo Vera alijibu kwa kicheko na mshangao.

Shabiki huyo alikuwa ameandika, “Huyo mtoto anakaa Otile niaje” na Vera anamjibu kirahisi tu kwa kicheko.

Vera Sidika
Image: Instagram screenshot

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza sura na muonekano wa Asia kuzua utata mitandaoni ambapo baadhi ya mashabiki walisema alikuwa ametumia mafuta yanayofanya nywele kuwa laini kwa mtoto wake, madai ambayo mama huyo wa mtoto mmoja alikanusha.

Madai haya ya kuhusishwa kwa sura ya mtoto wake na msanii Otile Brown yanakuja saa chache tu baada ya Otile kumpasha mtu anayedhaniwa kuwa Vera katika ukurasa wake wa Instagram alipopakia maandishi akimtaka aache kutaja jina lake katika maongezi yake na badala yake aheshimu ndoa yake.

Watumiaji wengi wa mitandao walisema maneno haya yalikuwa yanamlenga Vera ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akizungumza kwamba wana uhusiano mwema tu na wanaume wote ambao amekuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi siku za awali.