DJ Shiti atumia wimbo kujibu madai ya kutoa 150 kwa malezi ya mwanawe

Muhtasari

• DJ Shiti ameamua kujibu madai ya aliyekuwa mkewe kwamba anatoa shilingi 150 kwa malezi ya mtoto

• Ametunga wimbo kwa jina Drama za Mama Mariam ambo amemshirikisha msanii Sadii na kuamua kujibu madai hayo kupitia vina vya tafsiri

DJ SHITI
Image: Instagram

Mchekeshaji DJ Shiti hatimaye ameamua kuweka wazi kuhusu madai ya aliyekuwa mkewe na mzazi mwenziye kwamba mcheshi huyo anatuma shilingi 150 za Kenya kama ada ya malezi kwa mwanao.

Ila kinachochekesha Zaidi ni kwamba DJ Shiti ametumia wimbo kujibu madai hayo na kuwataka watu wanaoeneza madai hayo kwamba wasikuwe na haraka ya kueneza uvumi bila kusikiza pande zote mbili.

Wawili hao wamekuwa wakipapurana mitandaoni kuhusu malezi ya mwanao huku aliyekuwa mkewe Fash Hussein akisema kwamba tangu watengane DJ Shiti hajawahi shughulikia mwanao na ambacho amekimudu kutoa ni shilingi mia hamsini peke yake.

DJ Shiti alipohojiwa na wanablogu kuhusu madai hayo, alidinda kuyazungumzia na kusema kwamba ni mambo ya faragha na hawezi kuyazungumzia hadharani ila akasisitiza kwamba yeye anajua vyema anashughulikia malezi ya mwanake kama baba mzazi na kumkashfu aliyekuwa mkewe kwamba yeye ndiye mchawi na pindi mwanao atakapokuwa atamueleza mchawi ni nani, mkewe kwa kumjibu alisema kwamba mchawi ni yeye, kwani tangu lini mia hamsini pesa za Kenya zikalea mtoto.

Katika wimbo huo ambao Shiti ameupa jina ‘Drama za Mama Mariam’ anasema kwamba anahisi vibaya kwani hakupewa nafasi ya kujieleza na wengi walimsikiliza na kumuamini aliyekuwa mkewe.

“Yaani hii dunia mwenye ameongea wa kwanza ndiye anasikilizwa, 150, inaezalea mtoto surely?” anasikika akiuliza Shiti.

Pia amewashauri wanablogu kuwa wapole na kutokimbilia maneno tun a kuyaanza kuyaeneza bila kujua kiini chake ni kipi na ukweli wa mambo ni upi haswa.

“Na nyinyi keyboard worriors, msikuwe wepesi wa kueneza propaganda. Na ndugu zangu mablogas jamani, ndugu zangu, si msikizage pande zote,” anaimba DJ Shiti.