Je unaifahamu historia ya bendera Diamond alitumia kwenye wimbo wake?

Muhtasari

• Maoni kinzani yametolewa ndani na nje ya ukanda wa Afrika mashariki kuhusiana na video mpya ya msanii Diamond Platnumz, Gidi inayoonyesha bendera ya kibaguzi almaarufu Confederate flag.

Diamond Platnumz
Image: BBC

Maoni kinzani yametolewa ndani na nje ya ukanda wa Afrika mashariki kuhusiana na video mpya ya msanii Diamond Platnumz, Gidi inayoonyesha bendera ya kibaguzi almaarufu Confederate flag.

Bendera hiyo ya Confederate ya nchini Marekani ambayo inaashiria kile wazungu wanaitwa White Supremacy kwa maana kwamba bendera hiyo ikionekana moja kwa moja inazua ujumbe unaosema kwamba wazungu ni watu wenye thamani kuliko watu wenye rangi ya ngozi tofauti nao.

Bendera hii ya Confederate ina historia mbaya sana kwa Wamarekani Weusi na ilipoonekana tu tayari shirika la habari la BBC limeripoti kwamba kuonekana kwake kumezua ukosoaji mkubwa mitandaoni nchini Marekani.

Bendera hiyo inawakumbusha Wamarekani Weusi vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka kati ya mwaka wa 1960 na 1961 ambapo majimbo 11 kutoka kusini mwa Marekani yalijitenga na kuunda muungano wa ‘Cofederate State of America’ ili kupinga kuondolewa kwa utumwa ambapo walishabikia biashara ya watumwa Weusi na hapo wakajitenga na kuunda muungano ulioitwa Confiderate.

 Vita vilizuka ambapo mashirika mengi yalikuwa yalijumuika kupinga kuendelea kwa utumwa wa watu Weusi, kitu ambacho majimbo haya kutoka kusini yalikuwa yakitaka kiendelee. Baada ya vita vya muda mrefu majimbo haya yalishindwa na bendera yao hiyo ya Confederate ikachukuliwa na kuwekwa kama nembo ya urithi iliyowakilishwa utumwa na ubabe wa watu wenye rangi nyeupe.

Bendera hiyo ya ubaguzi wa rangi inahusishwa sana na watu wabaguzi wa rangi wanaojulikana kwa kizungu kama ‘neo-narcists’ na ‘far right extremists’ kama kitu cha kuwatishia Wamarekani wenye asili ya Kiafrika.

Kwa maelezo haya, bila shaka Wamarekani Weusi hawawezi furahia jambo hilo wanapoona bendera hiyo kwenye video ya msanii wa Kiafrika kwa sababu ina  tafsiri ya moja kwa moja kwamba ameungana na wababe hao katika kuwapiga vita ndugu zake Weusi.

Watu mbalimbali wamemshauri msanii Diamond Pamoja ya uongozi wake kuhariri upya video hiyo na kutoa sehemu ambazo zina muonekano wa bendera hiyo kwani hili litakuwa jambo zuri tena la busara kwa msanii kama yeye ambaye anapalia kutoboa tundu katika soko la muziki la Marekani.

Simulizi Na Sauti