Nilimvumilia Terrence sana, hakuwa na ndoto maishani - Milly Chebby

Muhtasari

• Mwanablogu Milly Chebby amesima kwamba alipitia kipindi kigumu katika miaka mitano ya kwanza katika mahusiano na Terrence Creative.

• “...Aki Terrence hakuwa na ndoto, hakuwa na maono, alikuwa tu,” Chebby alisema.

Image: INSTAGRAM// MILLY CHEBBY

Mwanablogu Milly Chebby amesima kwamba alipitia kipindi kigumu katika miaka mitano ya kwanza katika mahusiano na Terrence Creative.

Akizungumza katika mahojiano na Diana Marua, Chebby alisema kwamba ilikuwa vigumu kwake kufanya uamuzi kuingia kwenye ndoa na mchumba wake kwa kile alikitaja kuwa Terrence hakuwa na ndoto wala mwelekeo katika maisha.

“...Aki Terrence hakuwa na ndoto, hakuwa na maono, alikuwa tu,” Chebby alisema.

Aidha Chebby alisema kwamba mumewe alikuwa akitumia asilimia kubwa ya pesa zake katika uchezaji kamari, jambo ambalo lilipelekea yeye kutokubali kupata mimba kwa kuwa hakuwa na uhakika iwapo Terrence angekubali kuchukua kikamilifu majukumu ya kulea mtoto wao.

Licha ya changamoto zote walizozipitia, Milly Chebby amekiri kwamba Terrence Creative amebadilika na kuwa mtu mzuri na kwamba anamshukuru Mungu kwa zawadi hiyo, na kwamba hajuti kumvumilia mumewe.

Wawili hawa kwa sasa wanazidi kuwamotisha vijana wengi ambao wangependa kuingia katika maisha ya ndoa, huku wakizidi kupiga hatua kubwa katika sekta ya sanaa.