Waliniambia ninazaa kama panya - Diana Marua

Muhtasari

• Mwanablogu ambaye pia ni msanii chipukia, Diana Marua amesema kwamba mashabiki walimkejeli wakati ambapo alifanikiwa kupata watoto na mumewe Kevin Bahati, wakimwambia ‘kwamba anazaa kama panya.’

• Marua alisema kwamba kauli hizo za mashabiki ziilimfanya kuwa na msongo wa mawazo , kwa kuwa alishindwa cha kufanya ili watu hao kukoma kuingilia maisha yake.

Image: INSTAGRAM// BAHATI

Mwanablogu ambaye pia ni msanii chipukia, Diana Marua amesema kwamba mashabiki walimkejeli wakati ambapo alifanikiwa kupata watoto na mumewe Kevin Bahati, wakimwambia ‘kwamba anazaa kama panya.’

Akizungumza kupitia video aliyoipakia katika akaunti yake ya YouTube, Marua alisema kwamba kabla apate mtoto wake wa kwanza na Bahati, mashabiki walichukua wakati mwingi kumwambia kwamba anatakiwa kupata mtoto wake binafsi na kukoma kumlea mtoto wa aliyekuwa mpenzi wa Bahati.

Hata hivyo baada ya kuchukua hatua ya kuamua kupata mtoto, mashabiki haohao tena walianza kumkejeli wakimwambia kwamba anazaa watoto wengi kama panya.

Marua alisema kwamba kauli hizo za mashabiki ziilimfanya kuwa na msongo wa mawazo , kwa kuwa alishindwa cha kufanya ili watu hao kukoma kuingilia maisha yake.

Aidha, alisema kwamba Bahati alimsaidia sana kukabiliana na changamoto hizo na kumhakikishia penzi la kudumu.

Ametoa ombi kwa kina mama wengine ambao ni maarufu kutozingatia maneno yanayosemwa na mashabiki na badala yake kufuata ndoto zao bila kushurutishwa.