"Nikikosa Instagram jua muda huo niko na mwanangu Asia" - Vera Sidika

Muhtasari

• Vera Sidika amewaambia wafuasi na mashabiki wake kuwa akikosa kuonekana Instagram basi wasihofu kwani muda huo anautumikia na mwanawe Asia.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti na mfanyibiashara Vera Sidika ameusifia ukuaji wa haraka wa mwanawe Asia Brown na kusema kwamba tabasamu lake ni kamili ambalo huchukua muda wake mwingi kukaa tu akimtazama na hata kusahau kuingia kwenye mtandao wa Instagram.

Sidika amesema kwamba iwapo mtamkosa kwenye mtandao wa Instagram, muda mrefu kinyume na kawaida yake basi jua muda huo anautumikia kuwa na mwanawe Asia na mumewe Brown Mauzo.

“Nimetekwa sana na tabasamu la mwanangu Asia. Nikosapo kwenye mtandao wa Instagram, basi jua muda wangu huo nautumikia nikiwa na mwanangu Asia. Kihalisia, huwa niko na mwanangu na babake 24/7. Anacheza sana na muda wote anatabasamu,” aliandika Sidika kwenye instastories zake.

Mwanasosholaiti huyo pia amesema anasubiri sana mwanawe akue kwa haraka ili kuwa na ziara rasmi Pamoja huku wakifananisha vitenge kama mapacha.

Kuwa na familia ni raha iliyotukuka na kutakatika.