Ben Pol asifia mafanikio makubwa ya tamasha la Harmonize

Muhtasari

• Ben Pol amesifia tamasha la Afro East Carnival la Harmonizxe lililofanyika kwa mafanikio makubwa wikendi iliyopita.

• Amewataka wasanii kuunga mkono vitu vinavyoleta tija kama hivyo ili kukuza muziki zaidi.

Ben Pol
Image: Instagram

Msanii Ben Pol amelisifia tamasha la Afro East Carnival lake msanii mwenzake kutoka bongo Harmonize kwa kusema kwamba hajawahi ona tamasha la kufana kama hilo la Harmonize lililofanyika wikendi iliyopita huko Tabata Shule nchini Tanzania.

Nguli huyo wa mtindo aina ya RnB alikuwa mmoja kati ya wasanii waliosimamisha umati mkubwa kutokana ya ‘performance’ ya kupigiwa mfano katika tamasha hilo.

Pol alimsifia sana Harmonize kwamba licha ya pingamizi na changamoto kibao kutoka kwa wasanii mbalimbali waliokuwa wakimpiga vijembe lakini alifanikisha tamasha ambalo kulingana na yeye ni kubwqa Zaidi na ambalo halijatokea Tanzania mzima.

Vile vile amewataka wasanii na mashabiki kujitoa nje kabisa na kupiga sapoti vitu na mambo ambayo yanaleta faida, tija na muamko mpya katika tasnia ya Sanaa sit u nchini Tanzania bali Afrika Mashariki kwa ujumla.

Sijaona carnival kama ya Harmonize Afrika Mashariki, wakati mwingine ni bora mifumo ivunjwe tusapoti, mimi hata asingenialika angenikuta hapa,” alisema Ben Pol kulingana na gazeti la Ijumaa nchini Tanzania.