Harmonize arekebisha mambo baada ya Jux na Darassa kuteta

Muhtasari

• Msanii Harmonize ametoa orodha mpya ya mastaa na wasanii watakaohudhuria na kutumbuiza kkwenye tamasha lake la Afro East Carnival mwezi Machi.

• Haya ni baada ya Jux na Darassa kuteta vikali baada ya kuorodheshwa kwenye hilo bango pasi na kushirikishwa kwao.

Darassa, Harmonize na Jux
Image: Facebook

Msanii Harmonize ametoa orodha mpya ya mastaa na wasanii watakaohudhuria na kutumbuiza kkwenye tamasha lake la Afro East Carnival mwezi Machi.

Katiki orodha hiyo mpya, Harmonize hajawaorodhesha wasanii Jux na Darassa baada ya wawili hao kuteta vikali kwamba Harmonize aliwaorodhesha pasi na kuwahusisha wala kuzungumza na usimamizi wao binafsi wa kazi za Sanaa.

Jux alimjia juu Harmonize baada ya kubaini kwamba jina lake limeorodheshwa kwenye bango la tamasha hilo bila kutaarifiwa.

“Tafadhali hakikisha kuna makubaliano kati ya uongozi wangu na timu yako kabla ya kuniweka kwenye mabango ya matangazo kama haya. Tunapenda kushirikiana kama wasanii ila taratibu za kiuongozi zifuatwe,” Jux aliteta kwenye bango hilo lililopakiwa Instagram ya Harmonize.

Kwa upande mwingine, msanii Darassa pia amemjia juu Harmonize kwa ghadhabu kwani alipokea taarifa za jina lake kuonekana kwenye bango hilo kwa mshtuko mkubwa kwa sababu hakuwa ametaarifiwa wala kupewa mwaliko maalum.

“Kama artist, nina amini kwenye support lakini. Lakini vitu kama hivi lazima tuwe na mawasiliano before kufanya action kama hizi. Kuna ratiba zetu za kazi unaziweka…” alilalama Darassa.

Image: Instagram

Hatimaye msanii Harmonize alisakamwa na shinikizo huku wengine wakimsimanga na ikabidi akaliondoa bango hilo kwenye mtandao na baadae akalipakia lingine jipya pasi na majina ya wasanii hao wawili.