H-Baba ame unfollow Harmonize Instagram, kunani?

Muhtasari

• Msanii H-Baba Februari 9 ame unfollow bosi wake Harmonize kwenye mtandao wa Instagram na kumfollow Diamond Platnumz.

• Kisa hiki kinajiri saa chache tu baada ya msanii H-Baba kupakia video za Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshabikia kwa kutumbuiza Grammy

Harmonize, H-Baba na Diamond
Image: Facebook

Waswahili wanakwambia kangaja huenda yakaja na ukistaajabu ya Musa basi ya Firauni yamo njiani.

Msanii H-Baba Februari 9 ame unfollow bosi wake Harmonize kwenye mtandao wa Instagram na kumfollow Diamond Platnumz.

Kisa hiki kinajiri saa chache tu baada ya msanii H-Baba kupakia video za Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshabikia kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kutumbuiza kwenye hafla ya Grammy Global Spin iliyofanyika usiku wa kuamkia jana.

Wadadisi wa mitandaoni wanahoji kwamba huenda baada ya Harmonize kuona H-Baba akimshabikia Diamond ambaye ni mbaya wake Kondeboy, alikorofishana naye kuhusu suala hilo, jambo ambalo lilipelekea H-Baba kuchukua maamuzi ya ku unfollow na badala yake kum follow Platnumz, katika kitendo cha kumlisha nzi wa kijana bosi wake Harmonize.

Baada ya kitendo hicho ambacho wengi wamestaajabishwa nacho, msanii H-Baba ameenda kwenye Instagram yake na kuachia ujumbe mrefu unaonekana kama mpasho kwa mtu ambaye hajamtaja ila wengi wanahisi maneno hayo yanamlenga msanii Harmonize.

Amesema kwamba yeye katu hawezi kushawishika kufanya vile ambavyo hataki na pia akasema ukurasa wa Instagram ni wake na ana haki ya kupakia chochote atakacho.

“Mnatakiwa mjifunze mimi ninamaisha yangu binafsi nimeridhika nayo Sina ninacho nichakwangu sijashawishiwia namtu yoyote KUMPOST Simbaaa @diamondplatnumz nimimi mwenyewe nakihelehele changu kama anafanya poa kwanini nisimpost waswahili Wanasema maneno kibao narudia MSUKUMA anunuliwi wala hanunuliki ata sikumoja mimi sio muajiliwa wa mtu ni Mwanamuziki pia nishabiki kama Mwanamuziki mwenzangu kaupiga Mwingi nisiseme nasema kwa Hili @diamondplatnumz kaupiga Mwingi... Umeuwaaaaaah ATI nini Ameuwaaaah ATI niniiii Ameuwaaaaah JESHI LA MTU MMOJA NDIO MIMI #RAIS WA INSTA NDIO MIMI @h.baba_ Wengine fake fake KOSA LANGU NI KIHELEHELE CHANGU MWENYEWE PAGE NI YAKWANGU SIPANGIWIIIIIIII MIMI SIO CHAWA MIMI NISHABIKI MKUBWA NIKIKUBALI NIMEKUKUBALI KUTOKA MOYONI NAJITOA KUFA AU KUPONA....” ameandika H-Baba

Ikumbukwe msanii huyo mkongwe kwenye tasnia ya bongo fleva aliletwa tena upya kwenye mtanange huo na msanii baada ya kukaa kimya kwa muda. Harmonize alimleta kwenye mchezo na kumshirikisha katika kibao ambacho walishirikiana na msanii kutoka Kongo, Awilo Longomba, kibao kwa jina #Attitude.