Mimi sio Mmakonde mtu anisaidie nimseme vibaya - Uchebe amchamba Harmonize

Muhtasari

• Muigizaji na mmiliki wa karakana ya magari Uchebe ameonekana kumpiga vijembe Harmonize alipotolea mfano kwamba yeye si Mmakonde anayesaidiwa na kumsema vibaya aliyemsaidia.

Uchebe, Harmonize
Image: Instagram, Facebook

Muigizaji na mmiliki wa karakana ya magari nchini Tanzania Ashraf Sadiq almaarufu kwa jina la kisanii kama Uchebe amemchimba mikwara msanii Harmonize katika hafla moja alipokuwa akizinduliwa kama mmoja wa waigizaji wa tamthilia nchini humo.

Uchebe ambaye ni mumewe wa zamani wa mwanamuziki Shilole alikuwa akizungumza na wanahabari kabla ya kusaini mkataba wa ubalozi ambapo alisema kwamba siku zote anawalipa wema na fadhila wale wote waliomshika mkono na kumpa shavu wakati anakwea ngazi za maisha mpaka kufikia hatua alipo sasa hivi kwamba anaweza akaaminiwa na brand kama kubwa kama muigizaji nguli.

Katika kile kilichoonekana kama kumchamba Harmonize wazi, Uchebe alisema kwamba yeye hawezi kuwa kama mtu wa kabila ka Wamakonde ambao wanasaidiwa kuvuka mto kisha baadae wakifika ng’ambo ya pili wanamsukuma aliyewasaidia kuvuka na kumzamisha majini.

“Labda nikueleweshe kitu kimoja, na kitu ambacho katika dini yangu ninakiheshimu sana ni mtu anayenitoa hapa na kunipeleka sehemu nyingine. Nikitolea mfano hai, mimi sio kama Mmakonde kwamba mtu aliyenitoa nianze kumsema vibaya, siwezi!” alisema Uchebe.

Alikuwa akilijibu hili akizungumzia ni kwa nini siku zote anamheshimu Shilole hata baada ya mahusiano yao ya kimapenzi kuvunjika muda mrefu lakini akasema anamheshimu kwa sababu Shilole alikuwa kwenye Sanaa ya Bongo Movie kabla yake na ndio maana akipata dili kama hizo bado atamshirikisha kwai le heshima kwamba ni yeye alimtoa katika karakana na kumtambulisha katika Sanaa.

Kwa kuzungumzia Mmakonde watu wengi walihisi anamlenga Harmonize ambaye ni wa kabila la Makonde na ambaye alikuja kugeuka adui wa msanii Diamond baada ya msanii huyo kumtoa kimuziki.