Harmonize na Diamond Platinumz 'watiana vidole' kunani?

Muhtasari

• Msanii Harmonize ametangaza rasmi kwamba atakuwa anaachia kibao chake kipya #Bakhresa tarehe 12/3/2022.

• Muziki huo unakuja siku moja tu baada ya Diamond Platinumz kuachia Ep yake huku wengi wakizidi kulinganisha nguvu za wasanii hao wawili.

 

Harmonize na Diamond
Harmonize na Diamond
Image: INSTAGRAM

Msanii Harmonize ametangaza rasmi kwamba atakuwa anaachia kibao chake kipya #Bakhresa tarehe 12/3/2022.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amepakia kipande kifupi cha wimbo huo huku akisema kwamba anataka mashabiki 10,000 ‘kucomment’ ili aachie kibao hicho.

Muziki huo unakuja siku moja tu baada ya Diamond Platinumz kuachia Ep yake huku wengi wakizidi kulinganisha nguvu za wasanii hao wawili.

Ifahamike kwamba Harmonize alitarajiwa kutoa kibao hicho tarehe 4/3/2022, ambapo pia Simba alitarajiwa kutoa EP yake  ila akabadilisha kwa kile kilichosemekana kuzingatia maandalizi ya hafla yake ya Afro Canvo.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mvutano kati ya ‘Simba’ na ‘tembo’, kuhusu nani mkali kimuziki huku mashabiki wakiwa na maoni tofautitofauti.

Inasubiriwa kuona kati ya EP yake Diamond Platinumz [FOA] na kibao chake Harmonize[Bakheresa] gani itafanya vizuri.