Gharama zilikuwa kubwa, faida hamna! - mwandaaji Afro East Carnival

Muhtasari

• Hata kama wengi wanasema tamasha la Harmonize la Afro East Carnival lilikuwa na mafanikio makubwa, bado wandaaji wa tamasha hilo wanasema gharama ilikuwa kubwa na haiwezi rudi.

• Wanasema walifanya tu kwa sababu ya mapenzi yao kwa muziki wa bongo fleva.

Afro East Carnival
Image: Instagram

Mmoja wa viongozi kutoka rekodi lebo ya Konde Gang na muandaaji wa tamasha la Harmonize la Afro East Carnival ameweka wazi kwamba maandalizi ya tamasha hili yaligharimu kiasi kikubwa sana cha pesa ambazo hata mapato yenyewe hayawezi kukidhi.

Tamasha hilo lililofanyika wikendi iliyopita limepata sifa kochokocho kutoka kwa wapenzi mbalimbali wa muziki kwa mafanikio makubwa lakini walioliandaa bado wanasema halikufikia kiwango cha faida na hili walikuwa wamelitarajia na kusisitiza kwamba walifanya hivo si tu kwa kutaka faida bali kutokana na mapenzi ya dhati kwa muziki wa bongo fleva.

“Hata tungefanya kiingilio shilingi 50,000 na uwanja ungejaa bado gharama za maandalizi ni kubwa, tunafanya kwa ajili ya branding ya muziki wetu,” alisema kiongozi huyo katika mahojiano na wanahabari.

Tamasha hilo liliwavutia wasanii zaidi ya 40 kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania ambapo tamasha lilikwenda shwari kulingana na ratiba licha ya changamoto za muda na mambo mengine madogo madogo ambayo yanatajwa kuwa ya kawaida.

Msanii Harmonize ni mmoja kati ya wasanii wa bongo fleva ambao wanazidi kuzikwea ngazi za juu Zaidi kimuziki huku akiwa tayari ashaachia albamu mbili tangu ujio wake kwenye muziki kando na kumiliki rekodi lebo yake ya Konde Gang ambayo inatajwa kuwa namba mbili kwa ubora nchini humo nyima ya ile yam baya wake Diamond Platnumz ya WCB Wasafi ambayo pia ndiyo iliyomlea na kumtoa kimuziki.