Hata nikifariki naomba Wasafi muwe na umoja - Diamond

Muhtasari

• Diamond Platinumz amesema kwamba hajui atafariki kwa njia gani.

• Amekiri kwamba angependa kuiona Wasafi ikiendelea kusimama hata baada ya kuondoka kwake.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Diamond Platnumz

Afisa mkuu mtendaji wa Wasafi Media na msanii, Diamond Platnumz amesema kwamba angependa kuiona kampuni hiyo ikizidi kufanya vizuri hata baada ya kuondoka kwake.

Diamond amesema kifo ni jambo lisilotabirika na kwa hiyo hajui atafariki lini wala kutokana na nini.

Msanii huyo alisema angetaka kuona wafanyikazi wote wakifanya kazi kwa amani na kushirikiana kutimiza malengo yao binafsi na yale ya chombo hicho cha habari.

Akizungumza katika mahojiano ndani yakipindi cha #The Switch, Simba alisema kwamba wakati mwingi mwanzilishi wa jambo anapoondoka, wanaosalia wanakosa kufuatilia ile ndoto kwa bidii ile ile.

Simba ni moja kati ya wasanii ambao wanazidi kufanya mambo makubwa nje ya muziki, huku akizidi kutoa changamoto kwa wasanii wengine ambao wanategemea kazi zao za muziki tu ili kuendesha maisha yao.