Ringtone Apoko achapisha orodha yake ya watu mashuhuri matajiri zaidi Kenya

Muhtasari

•Ringtone amedai kuwa anamiliki majumba matano ya kifahari katika maeneo ya Runda, Karen na Muthaiga.

•Anerlisa Muigai, Khaligraph, KRG the Don, Betty Kyalo, Huddah Monroe, Otile Brown, DJ Moh na Size 8 pia wamefuzu katika orodha ya Ringtone.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Mwimbaji wa nyimbo za injili Ringtone Apoko amechapisha orodha yake ya Wakenya wenye umri mdogo ambao anaamini ni matajiri zaidi.

Mwanamuziki huyo ambaye anajulikana kujipiga kifua kuhusu utajiri wake amedai kwamba ndiye anayeongoza orodha hiyo inayojumuisha wasanii 12.

Katika orodha yake, Ringtone amedai kuwa anamiliki majumba matano ya kifahari katika maeneo ya Runda, Karen na Muthaiga. Vile vile ameongeza kuwa anamiliki magari saba ya kifahari yakiwemo Range Rovers, Mercedes -Maybach, BMW na kadhalika.

Wanaofuata  katika orodha yake ni wasanii wenzake Akothee na Jaguar.

"Akothee ana jumba moja la kifahari Mombasa na gari moja aina ya SUV, Jaguar ana nyumba mbili za kifahari na magari matatu, Bahati ana nyumba mbili za kifahai na magari matatu," Ringtone amesema.

Anerlisa Muigai, Khaligraph, KRG the Don, Betty Kyalo, Huddah Monroe, Otile Brown, DJ Moh na Size 8 pia wamefuzu katika orodha ya Ringtone.