Ni kuhusu kifo? Nandy ateta Instagram kudengua post zake

Muhtasari

• Mbona bwana insta hataki kabisa niongee ukweli wa moyo wangu. Instagram doesn’t want me to speak my truth - Nandy

Msanii wa bongo fleva Nandy
Msanii wa bongo fleva Nandy
Image: INSTAGRAM

Kwa wale mnaomfuatilia msanii Nandy kwa ukaribu bila shaka mtabaini msanii huyo amekuwa akipigana vita na suala fulani nafsini mwake ambalo linamtesa sana na anataka kulitema kwa kuliweka wazi, angalau apate amani ya nafsi.

Jumatatu msanii huyo alilalama kwamba mtandao wa Instagram ni kama hautaki kabisa kumpa ruhusa ya kupakia jambo hilo ili watu wajue, jambo lililodokeza uwezekano wa post zake kuhusu suala hilo kudenguliwa pindi anapofanya jaribio la kuzipakia.

Mbona bwana insta hataki kabisa niongee ukweli wa moyo wangu. Instagram doesn’t want me to speak my truth,” aliandika Nandy na kuambatanisha picha ya ilani kutoka Instagram kwamba post yake imeondolewa.

Baadhi ya wafuasi na mashabiki wake walihisi msanii huyo anatafuta kiki na kumtupia maneno lakini baadae aliwajibu kwa kuandika kwenye Instastories zake akisema yeye hana utoto wa kutafuta kiki kwa suala kama hilo.

Mpaka alidiriki kutaja kifo hapo kuwa miongoni mwa masuala ambayo amezuiwa na Instagram kuyaweka wazi ili watu wajue.

“Baadhi ya mafans wetu hawana kabisa Subira na jambo. Kila kitu wanachokiona wanaona ni kiki. Me nimesema nina jambo na jambo langu ni la kufundisha na si kuharibu. Nitafute kiki ya kufa nipost me mwenyewe? Mnahisi nina utoto kwa brand yangu kwa kiasi hicho?” aliteta Nandy kwa mashabiki wake.

Vile vile aliwasisitizia wafuasi na mashabiki wake kuwa na Subira kwa sababu anazidi kukuna kichwa kutafuta jukwaa ambalo litampa nafasi kufungua ya moyoni ambayo tayari Instagram imemzimia taa za mchana.

“Sasa sijui tu niende redioni niongee. Au niingie insta live. Au nifanyeje? Maana hili jambo linanitesa na limewatesa wengi sana. Ifike mahali itoshe, sio lazima kwani lazima…” aliandika Nandy kwenye instastories zake.

Unahisi ni jambo gani hili linalomzungusha kichwa binti mfalme wa muziki wa Afrika? mbona Instagram wanazishusha post kama hizo anazojaribu kupakia?