Hatimaye Steve Nyerere amejiuzulu kuwa msemaji wa wanamuziki

Muhtasari

• Hatimaye Steve Nyerere  Ijumaa amejiuzulu kama msemaji wa wanamuziki katika taifa la Tanzania.

• "...Nimejiuzulu kwa sababu sioni kama hizi kelele zina tija kwa taifa," Nyerere alisema.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Steve Nyerere

Hatimaye Steve Nyerere  Ijumaa amejiuzulu kama msemaji wa wanamuziki katika taifa la Tanzania.

Akizungumza katika ofisi za BASATA, Nyerere alisema kwamba taifa lina majukumu mengine makubwa ya kushughulikia badala ya kuendeleza mvutano wa kuteuliwa kwake.

"...Nimejiuzulu kwa sababu sioni kama hizi kelele zina tija kwa taifa," Nyerere alisema.

Nyerere alisema kwamba ataendelea kuwepo katika maisha ya wasanii kwani bado ana nafasi za uongozi katika sehemu mbalimbali na ataendelea kuendesha na kuandaa matamasha yanayawalenga wasanii.

"...Sitaki kutoka kwa maisha yao, kwa sababu mimi siijui kesho yangu," aliongeza.

Alishikilia kwamba kwa sasa atazingatia kumsaidia rais mama Samia Suluhu kufanikisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo itakayowasaidia wananchi.

Aidha, hakukoma kuushukuru usimamizi wa shirikisho la muziki Tanzania kwa kumuaminia na kumteua katika nafasi hiyo.

Ifahamike kwamba kumekuwa na vuta nikuvute baina ya wanamuziki na shirikisho la wasanii Tanzania, huku wanamuziki wakipinga uteuzi wa Nyerere kama msemaji wao jambo lililopelekea BASATA kusitisha uteuzi huo.