Roma Mkatoliki asema Nyerere anatumika na viongozi

Muhtasari

• Roma Mkatoliki amesema kwamba kuna viongozi wenye nguvu nyuma ya uteuzi wa Steve Nyerere kama msemaji wa wanamuziki.

• Aliwataka mashabiki na wasanii kutolichukulia jambo hilo poa tu.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Roma Mkatoliki

Rapa matata kutoka Tanzania, Roma Mkatoliki amesema kwamba kuna viongozi wakuu serikalini ambao wapo nyuma ya uteuzi wa Steve Nyerere kama msemaji wa wanamuziki.

Mwanamuziki huyo alishikilia kwamba sio vizuri serikali kuwalazimishia wasanii kiongozi ambaye hawamtaki.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika mitandao yake ya kijamii, Roma alisema kwamba Stebe Nyerere amepewa nguvu nyingi na viongozi fulani serikalini, jambo linalomfanya avimbe.

Shirikisho la wasanii lilijitetea kwamba walimteua Nyerere kwa sababu anaweza kuwa daraja kati ya wasanii na serikali.

Ifahamike kwamba Nyerere alisema hatajinyakua mamlakani licha ya shinikizo kutoka kwa wasanii.

Aidha, aliwataka wasanii wote kuungana kupinga uteuzi huo kwa kile alichokitaja kuwa kuikosea tasnia ya muziki wa bongo heshima.

Roma alisema kwamba huenda madhara ya uteuzi huo yasionekane kwa sasa, ila miaka mitano ijayo wasanii watajua uzito wake.