Baha wa machacharia na mpenzi wake watarajia mtoto

Muhtasari

• Aliyekuwa muigizaji wa kipidi cha machacharia, Baha a mpezi wake wanatarajia mtoto.

• Ameonyesha furaha yake na kusema yuko tayari kwa jukumu hilo.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Baha

Aliyekuwa muigizaji katika kipidi cha Machacharia, Baha na mpenzi wake wanataria mtoto.

Kupitia picha aliyochapisha katika ukurasa wake wa Instagram ikionyesha mpenzi wake akiwa amebeba ujauzito, Baha alisema kwamba anasubiri kwa hamu kumkaribisha mwanawe.

"...Sijawahi kuwa na furaha kiasi hiki," Baha alisema.

Alisema kwamba yuko tayari kuchukua majukumu ya kumlea mwanawe kwani amekuwa akitamani kipindi hicho kuwadia.

Mashabiki nao hawakusita kutuma jumbe za kumpongeza kwa hatua hiyo, wakimtakia heri katika safari hiyo.

Kwa muda sasa Baha amekuwa haonekani akipakia picha zao za pamoja katika mtandao , huku sasa mashabiki wakikisia kwamba ujauzito huo ndo ulikuwa chazo.

Baha sasa anaingia katika orodha ya wasanii ambao wake zao wana ujauzito, na ambao wamepelekea kwenye mtandao wa Istagram kuoyesha furaha yao.