Nina mengi ya kuzungumza ila naomba unisamehe, Babalevo amwambia Uchebe.

Muhtasari

• Hatimaye Babalevo ameamua kumuomba Uchebe msamaha.

• Amemtakia kila la heri katika mishe zake za kimaisha.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Babalevo na Uchebe

Msanii Babalevo hatimaye amefunguka na kumtaka Uchebe kumsamehe kwa matusi yote aliyomlimbikizia,

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Babalevo alionekana kuwa mwenye hisia nyingi kwa mambo yote mabaya ambayo aliyasema kumhusu Uchebe.

"Nina vitu vingi vya kuongea, ila kwa sasa naomba niseme pole nisamehe sana," Babalevo aliandika.

Aidha, alimtaka kuendelea kujituma katika mishe zake na kumtakia heri maishani.

Mashabiki hawakuficha furaha yao huku wakimpongeza kwa kitendo hicho cha uungwana.

Kuna wale pia ambao walisema kwamba Babalevo alikuwa anatafuta kiki kupitia ujumbe huo.

Ifahamike kwamba Uchebe alikuwa mumewe msanii Shilole, ila baadaye ndoa yao ilisambaratika.

Kulikuwa na semasema kwamba Uchebe alikuwa akimtegemea Shilole, jambo ambalo lilipelekea watu wengi kumdhihaki na kumkejeli Uchebe.

Babalevo akiwa mwandani wa Shilole, alimpaka tope Uchebe na kuzungumzia alivyokuwa hastiki kuwa mume wa Shilole kwa sababu hakuwa na hela.