Walikuwa wanafuta miziki yangu, Pilipili wa Calif Records atoa ya moyoni

Muhtasari

• Msanii Pilipili amesema kwamba bado anazidi kuachilia muziki licha ya kwenda kimya kwa muda mrefu.

• Alizungumzia jinsi baadhi ya wasanii wa Calif records walikuwa wanampiga vita.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Pilipili

Aliyekuwa msanii wa Calif records, Pilipili amefuguka mazito ya moyoni aliyoyapitia kipindi alikuwa chini ya lebo hiyo.

Akizungumza na mwanablogu Mugai Eve, Pilipili alisema kwamba baadhi ya wasanii waliokuwa katika kambi hiyo walikuwa wanamfitini na kumpiga vita.

Pilipili aliweka wazi kwamba wasanii hao walikuwa wakifuta ngoma zake kwenye kompyuta baada yake kurekodi.

Aidha, alisema kwamba kuna kipindi wasanii hao walikuwa wanatia sauti zao kwenye yimbo zake bila yeye kujua halafu baadaye wanaziachia bila kumfahamisha.

"Kuna kipindi nilikuwa natoka studio, halafu nashtuka wameeka mistari yao kwa ngoma yangu  na wameachia bila idhini yangu," Pilipili alisema.

Aliweka wazi kwamba hakuwahi fikiria kuondoka Calif ila mazingira yaliyokuwepo yalimlazimu kujiondoa.

Hakusita kumshukuru mamake Clemmo [ambaye alikuwa msimamizi wa lebo hiyo], kwa kumtia moyo na kumhakikishia kila uchao kwamba mambo yangekuwa sawa.

Vilevile alisema kwamba kulikuwa na sheria nyingi ambazo zilikuwa zinatoa mazingira mazuri yeye kujieleza na hata kutoa aina fulani ya muziki ambao alikuwa aataka.

Kulingana naye, wasanii hao walikuwa wanamuona kama mpinzani wao badala ya kushirikiana ili kupeleka muziki wao mbali.

Aliwahakikishia mashabiki wake kwamba asharekodi miziki ya kutosha na wataaza kuifurahua karibuni.