Jua Cali asema Illuminati ni ndoto tu, haipo

Muhtasari

• Msanii wa Gengetone Jua Cali anasema illuminati ni kitu cha kufikirika tu na ni cha udanganyifu ambacho hakipo kabisa.

• Jua Cali amesema wasanii hawafai kuwa na imani kwamba kuna watu wanaolaghai wasanii, kwa sababu fikra hizo ni kama kuaminii illuminati, vitu ambavyo havipo kabisa.

Jua Cali
Image: Facebook

Msanii wa Gengetone Jua Cali anasema illuminati ni kitu cha kufikirika tu na ni cha udanganyifu ambacho hakipo kabisa.

Msanii huyo mkongwe katika Sanaa ya muziki nchini Kenya kwa Zaidi ya miongo miwili sasa anadai kwamba siku hizi wasanii wengi wanafukuzia umaarufu mitandaoni badala ya kufanya muziki kwa bidii. akizungumzia kuwepo kwa illuminati na wanaowahadaa wasanii, Jua Cali amesema  hadithi za kuwepo kwa illuminati ni kama ndoto za alinacha.

Akionekana kutoa ushauri kwa wasanii wanaochipukia kwenye Sanaa, Jua Cali amesema wasanii hawafai kuwa na imani kwamba kuna watu wanaolaghai wasanii, kwa sababu fikra hizo ni kama kuaminii illuminati, vitu ambavyo havipo kabisa.

Nairobi Gossip
Image: Instagram (screengrab)

“Njia pekee msanii anaweza vuna faida ya kazi yake ni kutia bidi kwa sababu mtu yeyote anaweza ona bidi na jitihada zako na pia kuwa dhabiti katika kazi zao,” Jua Cali alisema wakati wa mahojiano katika runinga ya NTV asubuhi ya Februari 3

Akizungumzia siri ya uwepo wake katika Sanaa kwa muda mrefu Zaidi, Jua Cali amesema, “Mimi naimba na kufoka jinsi ambavyo watu huongea. Hii inakuwa rahisi kwa watu kuimba Pamoja na mimi kwa sababu ni kama nachukua maneno kutoka mdomoni mwako halafu nayaimba.”

Madai haya yake kuhusu kutokuwepo kwa illuminati kunakuja siku chache tu baada ya muimbaji na mzalishaji wa nyimbo Magix Enga kuibua madai kwamba alijiunga katika kundi hilo na kisha baadae akakengeuka na kukana madai ya kujiunga kwenye kundi hilo.