Mnajipendekeza serikalini! Roma Mkatoliki awasuta wasanii

Muhtasari

• Roma Mkatoliki amesema kwamba wasanii wengi wa Tanzania wanajipendekeza kwa serikali.

• Amewataka kutambua umuhimu wa producers na mashabiki wao.

Rapa matata kutoka Tanzania, Roma Mkatoliki amewasuta vikali wasanii ambao wanajipendekeza kwa serikali.

Alikuwa akiyazungumza haya baada ya hafla ya tuzo za muziki zilizofanyika siku ya Jumamosi.

Roma aliwataka wasanii hao kutambua umuhimu wa mameneja, maproducer na mashabiki wao badala ya kuisifia serikali ambayo si sehemu kubwa ya ufanisi wao kwenye muziki.

"Msanii ukishinda tuzo, toa hotuba yako mshukuru Mungu, producer, vyombo vya habari, usimamizi na mashabiki. Haya mambo unapanda jukwaani halafu unaishukuru serikali sioni kama yanafaa," Roma aliandika.

Baadhi ya watangazaji na wacheza santuri pia walitupia kauli zao wakionyesha kushangazwa na kitendo hicho cha wasanii.

"Mi pia nimeshangaa sana aisee 😄 nikahisi labda sijaelewa 🤦‍♀️ ,dj mamieofficial aliandika.

Ifahamike kwamba tuzo hizo zilikuwa zinafanyika baada ya kuzama kwa zaidi ya miaka saba.