(VIDEO)"Mombasa Sirudi tena!" Sandra Dacha asema baada ya kuchezea mzungu densi bila mafanikio

Muhtasari

• Muigizaji Sandra Dacha aapa kutorudi Mombasa baada ya juhudi zake za kumchezea mzungu densi kugonga mwamba.

• Mzungu huyo muda wote alionekana amesimama tisti pasi na kuonesha hisia hata kidogo kutokana na densi ile.

Muigizaji Sandra Dacha akicheza densi
Muigizaji Sandra Dacha akicheza densi
Image: SANDRA DACHA//INSTAGRAM

Muigizaji na mchekeshaji Sandra Dacha Jumatatu aliwaacha watu katika mtandao wa Instagram wakicheka baada ya kuonekana kwenye video akijaribu kumchezea mwanaume mzungu densi lakini mwanaume huyo hakuonesha hisia hata chembe.

Katika video hiyo inayoakisi kabisa kwamab alikuwa anajaribu kumshtukizia mzungu huyo kama vile ambavyo mcheza densi maarufu kwenye mtandao wa TikTok, Moya David anavyofanya, Dacha alirambishwa garasa na mzungu baada ya jaribio lake kutozaa matunda jinsi ambavyo Moya anafanikisha katika densi zake.

Dacha aliwaza na kuwazua na kufikiria pengine ni vile yeye ni mkubwa wa umbile la mwili na pengine wazungu hawapendi watu wenye unene kiasi hicho.

Kwa kweli, alighadhabika!

“Sijawahi elewa ni kwa nini wazungu hawajawahi pendi vitu nono nono,” aliandika Sandra Dacha.

Pia aliapa kwamba hatowahi Mombasa tena kwa sababu yule mzungu alimkwaza kwa kutoonyesha hisia zozote licha yake kujitutumua kwa densi ja Moya David.

“Yaani juhudi zangu zote zimekunywa maji hivo! Mombasa sirudi tena!” aliandika Dacha.