Kizz Daniel achekwa kufika kwenye tamasha nchini Benin siku moja kabla

Msanii huyo alikuwa ametiwa mbaroni Tanzania kwa kuchelewa kuwahi katika tamasha la kulipwa.

Muhtasari

• Wiki mbili zilizopita, msanii huyo alitiwa nguvuni Tanzania kwa kukosa kutumbuiza licha ya kulipwa.

• Wengi walisema hatua ya kufika kwake siku moja kabla ilikuwa ni funzo kutokana na tukio hilo la Tanzania.

Msanii huyo alitiwa mbaroni nchini Tanxania kwa kukosa kutumbuiza licha ya kulipwa
Kizz Daniel Msanii huyo alitiwa mbaroni nchini Tanxania kwa kukosa kutumbuiza licha ya kulipwa
Image: Instagram

Wiki mbili zilizopita, Nyota wa Afropop wa Nigeria Kizz Daniel, aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi nchini Tanzania kwa kile ilisemekana kwamba alipokea pesa ila hakutokea kutumbuiza kama walivyoafikiana.

Mwanamuziki huyo alishindwa kujitokeza kwenye tamasha la kulipwa Jumapili usiku jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akifanyqa ziara ya kutambulisha ngoma zake kote duniani, ziara aliyoibatiza jina "Afro Classic World Tour"

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwimbaji huyo wa Nigeria na wenzake wanaonekana wakichukuliwa na maafisa wa polisi wa Tanzania kutoka hoteli ya Johari Rotana hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay, katikati mwa jiji.

"Nilikuambia jana ... nilikuomba kwa saa mbili, uombe msamaha kwa polisi sasa," sauti ya hasira inasikika ikisema.

Sasa nguli huyo wa kibao moto cha Buga wikendi iliyopita alikuwa na tamasha kama hilo nchini Benin ambapo kupitia Instagram yake alidokeza kwamba amewazili nchini humo siku moja kabla ya tukio lenyewe, taarifa ambayo wengi wa mashabiki wake waliipokea kwa mseto wengi wakionekana kumtania kwamba ameamua kuwasili saa 24 kabla ili kukwepa hali kaam iliyomtokea Tanzania isije ikajirudia.

“Benin nimetua salama, watu wakubwa, nguvu kubwa zaidi. Kesho usiku tuna buga, nawapenda sana,” Kizz Daniel alidokeza kweney Instagram yake akiashiria kufikia siku moja kabla.

Msanii mwenzake Davido alikuwa miongoni mwa watu wengine wengi waliomtupia utani huku wakimuambia kwamba amefika siku moja kabla kwa kupata funzo kutoka Tanzania ambapo alifika kuchelewa na hivyo kutofanikisha kufika kwenye tamasha alilokuwa amelipwa kutumbuiza.

“Ulifika siku moja kabla,” Davido aliandika huku akifuatisha kwa emoji za kucheka.