Mnaosema shoo yangu ni ya kitoto, hata Mungu anapenda watoto - Willis Raburu

Alisema wale wanaomsimanga mitandaoni hana haja nao kwani amezoea matusi na mara nyingine anawablock tu na kusonga mbele.

Muhtasari

• Raburu hivi karibuni alifichua kwamba alifanya upasuaji wa Gastric Bypass wa kupunguza uzito wa mwili.

• Alisema kabla ya kufanya upasuaji huo, alikuwa na kilo 164 ila azimio lake ni kufika uzito wa kilo 95.

Mtangazaji Willis Raburu amesema hana tatizo na watu wanaomtukana mitandaoni kuhusu shoo yake ya 10Over10
Mtangazaji Willis Raburu amesema hana tatizo na watu wanaomtukana mitandaoni kuhusu shoo yake ya 10Over10
Image: Facebook//WillisRaburu

Mtangazaji wa runinga Willis Raburu amezungumzia madai ya watu kumzomea kwamba anakuwa na tabia ya kitoto katika shoo yake ya 100ver10.

Alisema kwamba watu hao wanaomzomea na kumtukana kwamba shoo yake ni ya kitoto hawajui kwamba hapo ndipo anapata riziki yake na kusema kwamba yeye amekuwa akijua kwamba hawezi kumfurahisha kila mtu.

Alisema kwamba kazi yake anaikubali hata kama inaitwa ya kitoto kwani hata biblia yenyewe inasema kwamba Mungu anapenda watoto na yeye hana tatizo na kipindi chake kufananishwa na kipindi cha watoto.

"Hata wakisema shoo yangu ni ya kitoto ni sawa hakuna tatizo. Hata biblia inasema wacheni watoto wakuje kwangu. Mungu mwenyewe anapenda watoto," Raburu alimwambia Massawe.

Raburu ambaye juzi alifichua kwamba alilazimika kufanya upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili baada ya kujaribu kufanay mazoezi na ikashindikana, alisema mpaka leo hii bado watu wanamsimanga kwenye mitandao ya kijamii lkini suala hilo halimzuii wala kumfanya kujiona mtu baki.

Akizungumzia upasuaji huo, alisema kwamba si wa kawaida kwani mtu huwezi ukapasuliwa ngozi yako bali ni shimo ndogo tu inatobolewa.

Mtangazaji huyo aliyeshabikiwa sana alikuwa akizungumza kwenye redio Jambo na mtangazaji Massawe Japanni na alisema kwamba alifanya upasuaji huo mwezi Mei na mpaka sasa tayari amepunguza uzito wa kilo 21.

Raburu alisema awali alikuwa na uzito wa kilo 164 na sasa ako na uzito wa kilo 140 hapo. Alifichua kwamba matarajio yake ni kupunguza uzito wa mwili mpaka kufika uzito wa kilo kati ya 95 hadi 100 hapo itakuwa vizuri kwa upande wake.

Alisema upasuaji huo wa Gastric Bypass ulimfunga utumbo na kuzuia kiwango cha chakula ambacho anakila na kwamba mtu aliyefanyiwa upasuaji kama huo akizidisha kiwango cha chakula hakiwezi ingia kwani atakitapika.