Juzi nilipigwa kofi moja kali na baby mama - 2Mbili

2Mbili ni mzalishaji wa vipindi vya Obinna kwenye mtandao wa YouTube

Muhtasari

• Alisema baada ya kupigwa na kufichua kisa hicho kwenye Instastory yake, mtu wa kwanza kufika kwake alikuwa Oga Obinna rafiki yake.

Mchekeshaji 2Mbili asema alipogwa kofi na mzazi mwenzake
Mchekeshaji 2Mbili asema alipogwa kofi na mzazi mwenzake
Image: Instagram

Mchekeshaji 2mbili amefichua kwamba hivi karibuni alipigwa kofi moja la moto na mzazi mwenzake.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini, 2mbili alisema kwamab tukio hilo lilimtokea hivi juzi ambapo aliwataarifu mashabiki wake kupitia instastories.

Baada ya tukio hilo kumtokea, mtu wa kwanza kuona taarifa hiyo kwenye instastory yake alikuwa ni rafiki wake wa karibu, mchekeshaji Oga Obinna.

2mbili alisema kwamba kando na kuwa na ukaribu wa kikazi na Obinna ambapo anafanya kama mzalishaji wa vipindi vya Obinna kwenye mtandao wa YouTube, pia wao ni marafiki wakubwa sana kutoka mizizi ya kifamilia ambapo watoto wake wanamheshimu.

Obinna na 2mbili wana kitu kimoja cha kuwakutanisha ambacho ni kwamab wote ni wazazi lakini hawaishi pamoja na mama wa watoto wao.

“Juzi nilipata shida kwangu, nilipigwa kofi na mzazi mwenzangu, alinipiga vibaya sana na niliweka pale kwenye Instastory na chini ya dakika 30 mtu wa kwanza kufika kwangu alikuwa ni Obinna,” 2mbili alifunguka.

Akizungumzia Sakata la wiki chache zilizopita lililomhusisha Obinna na mzazi mwenzake pia aliyemwaga mtama kusema mchekeshaji huyo hashughulikii watoto, 2mbili alionekana akimtetea na kusema kwamba alikuwa anamtetea kwa sababu anabahatika kujua ukweli kidogo kuhusu Sakata hilo. Alisema ukaribu wake na watoto wa Obinna ndio ulimfanya kutaka kumtetea Obinna kutokana na madai ya mzazi mwenzake.

“Nikiona mtu kama Obinna ameingiliwa pale na mimi mwenyewe najua sehemu kidogo ukweli uko wapi lazima niingile kumtetea. Kwa sababu haiwezekani wewe ni mwanamke  na unaenda kumvua nguo baba wa watoto wako hadharani, na unajua ni uongo,” 2mbili alisema.