Nimekuwa kimapenzi na wanaume 10 hadi 15 hivi mpaka sasa kama sijakosea - Pritty Vishy

Vishy alisema ana miaka 20 na hivi karibuni anatarajia kusherehekea miaka 21.

Muhtasari

• Pia mwanadada huyo alidhibitisha kuwa mahusiano yake kimapenzi na msanii Madini Classic yaliisha muda mrefu.

Pritty Vishy asema yeye amechumbiana na wanaume kadhaa
Pritty Vishy asema yeye amechumbiana na wanaume kadhaa
Image: instagram

Mwanablogu wa YouTube Pritty Vishy amefunguka ukweli kuhusu mambo mengi katika kipindi cha maswali na majibu kati yake na mashabiki wake kwenye ukurasa wa Instagram.

Vishy ambaye umarufu wake ulikwea ngazi kwa haraka mno kutokana na ukaribu wake na msanii Stevo Simple alifichua kwamba hivi karibuni atatimba umri wa miaka 21 na kusema itakuwa siku yenye tafrija la kukata na kisu chenye makali kuwili.

Shabiki mmoja alimuuliza Vishy kama anaweza kufunguka kuhusus idadi ya wapenzi wa kiume ambayo amewahi kuwa nao kimapenzi tangu kubakehe na kujua mapenzi.

Mwanadada huyo asiyeficha aliwashangaza wengi baada ya kufunguka kuwa hawezi kukumbuka ila akakadiria kuwa huenda kama si 10 basi ni 15 hivi, idadi ambayo hakuwa na uhakika nao hata hivyo.

“Body count yako ni ngapi mpaka sasa,” shabiki mmoja alimuuliza.

“Waah ni ngumu kidogo lakini nafikiri kama si kumi basi ni kumi na tano hivi kama sijakosea,” Vishy alijibu.

Pia alipoulizwa mpenzi wake Madini Classic yuko Vishy, Vishy alijibu kwamba yeye hana mpenzi na kusisitiza kuwa yupo singo mpaka baadae sana, jibu ambalo liliwashangaza wengi kwani kila mtu alikuwa anajua yeye na msanii Classic ni kitu kimoja.

Pritty Vishy alijibu pia kuwa yeye hana mpango wa kupata mtoto kabisa katika kile alitaja kuwa ni jambo gumu sana kutokea katika maisha yake kwa sasa.

Alisema alikuwa ameolewa kitambo sana mpaka akatwangwa talaka na kuwa jambo la kuingia katika ndoa na kuwa mtiifu kwake ni kama mbinde.

“Nilikuwa nimeolewa kitambo mpaka nikapewa talaka. Sasa hivi sitaki upuzi kama huo kwa sababu kuwa katika ndoa na kuwa mtiifu ni kitu cha mwisho mimi ninaweza kukifanya,” Vishy alijibu.

Vishy katika majibu mengi alionekana kudokeza kuwa yeye na msanii Madini Classic hawako pamoja na kujuta kwamba katika siku za mbeleni kama atataka tena kuingia katika mapenzi basi hatofanya hivo na mtu maarufu bali litakuwa ni jambo la kisiri sana.

Anasema haya huku aliyekuwa mpenzi wake Stevo Simple Boy akiwa katika mchakato wa kufunga harusi na mpenzi wake Gee.