"Sitaki achanganyikiwe!" Pritty Vishy afichua kwa nini hatahudhuria harusi ya Simple Boy

Kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 alidokeza imani yake kwamba ndoa kati ya Stivo na mpenziwe haitadumu.

Muhtasari

•Vishy alibainisha kuwa hana nia ya kuvuruga harusi ya Stivo kwani kuwepo kwake huko kunaweza kumchanganya.

•Hivi majuzi Stivo alidokeza mipango ya kufunga pingu za maisha na mchumba wake hivi karibuni.

Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Image: SCREENGRAB// MUNGAI EVE

Aliyekuwa mpenzi wa Stivo Simple Boy, Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy amedokeza kuwa hatahudhuria harusi ya mwimbaji huyo wakati ambapo atakapiga hatua ya kufunga pingu za maisha.

Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram, kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 alibainisha kuwa hana nia ya kuvuruga harusi ya Stivo kwani kuwepo kwake huko kunaweza kumchanganya.

"Nikienda huko ataona matako zangu achanganyikiwe sasa sitaki hivo. Acha wafunge pingu polepole bila usumbufu," Vishy alisema.

Alikuwa akimjibu shabiki aliyetaka kujua ikiwa atahudhuria harusi ambayo Stivo amedokeza kufanya na mpenziwe wa sasa Jenny Wangui.

Vishy hata hivyo alidokeza imani yake kwamba ndoa kati ya wawili hao haitadumu.

"Najua penye hiyo pingu ya maisha itavujikia ata si kufunguka," Alisema.

Katika mahojiano ya hivi majuzi, Stivo alidokeza mipango ya kufunga pingu za maisha na mchumba wake hivi karibuni.

Haya yalijiri wiki chache tu baada ya mwanamuziki huyo kutoka Kibra kupiga hatua ya kumvisha pete ya uchumba Bi Jenny.

Vishy alikuwa miongoni mwa watu waliompongeza Simple Boy kwa hatua hiyo kubwa ambayo alipiga mwezi jana

"Kusema kweli nina furaha kwa ajili yao. Mimi nina furaha sana kwa ajili yake (Stivo) kwa sababu ata nilimove on. Kila mtu amemove on," Vishy alisema katika mahojiano na Eve Mungai.

Wakati huo, Vishy alimshauri mpenzi huyo wake wa zamani kuwa makini kuhusu masuala ya mahusiano na ndoa.

Pia alimsihi kuendeleza uhusiano mzuri wa kirafiki naye licha ya kuwa walitengana miezi kadhaa iliyopita.

"Ningependa awe rafiki yangu. Juu tuliachana haimaanishi tunafaa kuwa maadui. Huwezi kujua huko mbele tutasaidiana vipi. Ningependa awe rafiki yangu na apate mtu bora zaidi," Alisema.

Vishy pia alimshauri Stivo kumdekeza mchumba huyo wake na kumuonyesha mapenzi jinsi ambavyo wanadada hupenda.

Katika kipindi chake cha Q&A, muuzaji huyo wa nguo pia alipuuzilia mbali madai kwamba Stivo ndiye aliyemsaidia kupata umaarufu.

Vishy alisema kuwa umaarufu wake ulitokana na bidii kubwa aliyoweka na kubainisha kuwa yeye ndiye aliyemsaidia Stivo kuinuka.

"Niliufanyia kazi kwa bidii, watu ambao walikuwa karibu nami wakati huo wanaweza kutoa ushahidi. Badala yake anayeitwa msanii ndiye asiye na shukrani hapa," Alimjibu shabiki aliyemshtumu kwa kutokuwa na shukrani kwa Stivo.

Stivo na Vishy walitengana mwezi Machi mwaka huu baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu.