Si kama zako za maua mengi kama unashoot nyuki - Dimpoz amjibu Hanscana

Hanscana alikuwa amepinga kauli ya Ommy kuwa alifanya video yake Uhispania.

Muhtasari

• Ommy Dimpoz alipakia habari akisema alifanya video ya ngoma yake mpya Uhispania.

• Mwelekezi Hanscana akakanusha madai hayo akisema Ommy hakufanya video hiyo Uhispania.

Vita vya maneno baina ya Ommy Dimpoz na Hanscana
Vita vya maneno baina ya Ommy Dimpoz na Hanscana
Image: Instagram

Msanii Ommy Dimpoz baada ya kukaa kimya kimuziki kwa muda mrefu hatimaye amerejea na kitu kipya kwa jina Vacation.

Dimpoz alifichua kwamba alifanya vudeo ya dude hilo la moto nchini Uhispania katika eneo moja maarufu kwa jina Ibiza.

Msanii huyo mwenye majigambo si haba alitamba na kutanua kifua kwamba yeye ndiye msanii pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuweka rekodi ambazo hazijawahi wekwa tangu mataifa katika ukanda huu kujinyakulia uhuru.

Itakumbukwa msanii huyo ndiye alikuwa mtu wa kwanza kutoka ukanda huu kufika uwanja wa Old Trafford na kuchukua picha na wachezaji maarufu kama Christiano Ronaldo na wengine.

Sasa pia alisema kuwa ndiye msanii wa kwanza kutoka ukanda huu kufanya video ya ngoma katika eneo hilo la Ibiza nchini Uhispania.

Baada ya kusema hivyo, hili halikuenda sawa kwa baadhi ya wasanii ambao walimsuta vikali kuwa anadanganya kutafuta kiki tu kwa ngoma yake mpya,

Mwelekezi wa video nchini Tanzania, Hanscana alimjia juu vikali kwa kumwambia kuwa hakufanya video Uhispania bali ni klipu ndogo ndogo alifanya kwa simu na kuunganisha kusema ni video, jambo ambalo Dimpoz hakukawia kulijibu kwa kumsuta Hanscana kuwa video hiyo ni ya daraja la juu kuliko zile ambazo anawafanyia baadhi ya wasanii. Dimpoz alimkejeli kuwa zake ni za maua kama vile anavutia nyuki bila kuwa na ubora wowote.

“Hujashot, sema umechukua viklipu ukaunganisha na kuvibandika juu ya sauti ya muziki wako,” Hanscana alimwambia Ommy.

“Kaka hizi si zile video zako za maua mengi kama unashoot nyuki. Ukishapata viza twende ukaoshe macho kidogo,” Ommy Dimpoz alimjibu.

Msanii Baba Levo pia alionekana kutokubaliana na Ommy na hata kumtaka kupakia bajeti ya matumizi kwa kila kitu kwenye video hiyo iliyofanyiwa Uhispania, jambo ambalo Ommy Dimpoz aliahidi kuwa ataliweka wazi.