"Pesa hung'arisha!" Wanamitandao wasema baada ya Lulu kupakia picha ya zamani na Rashid

Rashid na Lulu ni wanandoa amabo pia wanajiongeza kama wanahabari wanaofanya kipindi kimoja runingani.

Muhtasari

• “Kuna mtu alikuwa anasema kitu, siku hizi hasemi kitu, mtaje,” Lulu alimtania Rashid.

Lulu Hassan apakia picha yake ya zamani ya mumewe Rashid
Lulu Hassan apakia picha yake ya zamani ya mumewe Rashid
Image: Instagram

Mwanahabari maarufu nchini Lulu Hassan amewachekesha wanamitandao baada ya kupakia picha ya zamani kabisa akiwa na mumewe Rashid Abdalla.

Katika picha hiyo inayowaonesha wawili hao wakiwa wameketi kwenye mkahawa mmoja, Lulu anaonekana akiwa ameangaza tabasamu lake huku mpenziwe Rashid akiwa ameangalia kando akiwa kwenye bahari ya mawazo, mtu asijue alikuwa anafikiria nini.

Kama hiyo haitoshi, Lulu alimtania Rashid kwa kauli yake ya ‘Sisemi Kitu’ na kusema kwamba kipindi hicho kuna mtu alikuwa anasema kitu lakini siku hizi hasemi tena, na kuwataka mashabiki wake kumtaja huyo mtu – bila shaka akiwa anamaanisha kumtania mumewe moja kwa moja.

“Kuna mtu alikuwa anasema kitu, siku hizi hasemi kitu, mtaje,” Lulu aliandika huku akifuatisha na emoji za kucheka.

Picha hiyo ya zamani iliwaonesha wakiwa katika hali duni ajabu kwenye kibanda umiza, jambo amablo liliwafanya baadhi ya mashabiki wao kuwatania kwamba kweli hela ndio sabuni ya kung’arisha kwa muosho mmoja.

“Je, alikuwa sawa? 😩 ama ni Njaa? Babes wewe ni wash wash peep maana umeosha kapsaa,” mwigizaji Kate Actress aliwatania.

“Hakuna mtu mwenye sura mbaya, ni umasikini uliomo ndani yake ndio unaowafanya waonekane na sura za kutisha,” mwanaharakati Boniface Mwangi aliandika.

Wengine waliwashabikia kuwa wapenzi wanaodumu pamoja katika hatua ngumu za maisha mabaya ya awali huishi milele kugandiana kama ruba.

Walitumia mfano huo na kuufananisha na ule wa rais William Ruto baada ya picha zao na mkewe kuibuliwa pia zikionesha maisha yao ya kimapenzi awali kabla ya utajiri na umaarufu.

Ama kweli, safari ya maisha huanza kwa hatua moja ya ujasiri!