"Maisha yalikuwa magumu" Kate Actress ajivunia maendeleo yake makubwa

Muigizaji huyo alisema alikuwa akikabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha kabla ya kuwa maarufu.

Muhtasari

•Kate alibainisha kuwa bado maisha yanampa changamoto ila sasa anaweza kukidhi mahitaji yake mengi na familia yake.

•Alifanyiwa mchakato wa  liposuction ambao ni mbinu ya kupunguza ukubwa wa mwili kwa kupima kiwango cha chakula ambacho mtu anakula kwa siku.

Kate Actress

Aliyekuwa muigizaji wa kipindi cha Mother-in-law na mshindi wa tuzo nyingi za uigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress ameanika picha zake za hapo awali kabla ya kujizolea umaarufu mkubwa.

Kate alikiri kuwa kipindi kile alikuwa akikabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha kabla ya kufanikiwa hatimaye.

Hii ilikuwa kabla ya kujitosa kwenye ndoa na mwelekezaji wa filamu, Phil Karanja, na kujifungua mwanawe wa pili.

Alibainisha kuwa bado maisha yanampa changamoto ila sasa anaweza kukidhi mahitaji yake mengi na familia yake.

"Wakati maisha yalikuwa yananishughulikia, usichanganyikiwe bado hayako sambamba ila sasa naweza kununua mvinyo mzuri," Kate alisema huku akiwatakia wanamitandao na mashabiki wake siku njema ya Utamaduni.

Pia alianika picha yake ya hivi karibuni akisherehekea siku ya Utamaduni kwa kuonyesha tamaduni ya wanawake Wakenya ya upishi.

Mama huyo wa watoto wawili amebadilika kiumbo baada ya muda huo wote na hata kuwa na muonekano mpya kwa upande wa mavazi na hata urembo.

Mwigizaji huyo alifanyiwa upasuaji baada ya kujifungua mtoto wake wa pili na kuongeza mwili ingawa hapo awali alikuwa mwenye mwili mdogo.

Kate alifanyiwa mchakato wa  liposuction ambao ni mbinu ya kupunguza ukubwa wa mwili kwa kupima kiwango cha chakula ambacho mtu anakula kwa siku.

Hata hivyo Kate alisema kuwa anapenda umbo lake hata awe mkubwa kiasi gani au mdogo kiasi gani baada ya kuonekana kuwa na mwili mdogo baada ya upasuaji wake.

Muigizaji huyo ameigiza kwenye vipindi mbalimbali vya Kenya kama Plan B, Sue na Jonnie na Disconnect na hivi majuzi alipata kandarasi katika  jukwaa la filamu la kimataifa, Netflix ambapo aliigiza kwenye filamu ya Birgerton.