Betty Kyalo amtungia mama yake ujumbe maridadi siku yake ya kuzaliwa

Betty alimsifia mama yake kuwa mama bora kwake na kuwa shabiki wake mkubwa

Muhtasari

• Betty alimshukuru mama yake kwa kuwa rafiki yake wa dhati na kumwelekeza kimaisha.

Betty Kyalo na mama yake

Mwanahabari Betty Kyalo amesherehekea siku ya kuzaliwa ya mama yake leo Alhamisi Oktoba 27.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Kyallo alipakia picha za kumbukumbu za mama yake na yeye na kusema jinsi anavyompenda na kumthamini.

Alimshukuru mama yake kwa kumuunga mkono wakati wowote na kumwelekeza kama binti yake ingawa yeye ni mtu mzima.

"Mama mpendwa. Heri ya kuzaliwa. Wewe ni malkia wa kweli . Wewe ni mfano bora unaoeleza nguvu na neema. Wewe ni mtu mrembo na mwenye roho safi. Utaishi kuwa shujaa wangu milele," mama huyo alisema.

Betty alizungumzia uhusiano wake na mama yake ambao ni wa karibu na alivyojfunza mengi kutoka kwake.

Alieleza jinsi mama yake ni mtu bora, si kwake peke yake bali kwa kila mtu anayehusika naye.

"Unapendwa na kuthaminiwa nami. Umenifunza mambo mengi makubwa na umeushika mkono wangu katika kila hatua ya safari yangu. Wewe ni shabiki wangu mkubwa kwa chochote ninachofanya. Unanipa uwezo wa kuendelea na kunishauri kila uchao," Kyallo aliandika.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kuwa anafahamu anachokitarajia sana mama yake katika maisha yake.

"Najua ombi lako kwangu na ninajua kuwa Mungu atakusikiliza! Nakupenda sana malkia wangu" Betty alisema.