'Alimlea kijana mkarimu,'Nyamu amsifia marehemu mamake Samidoh, asema watamkumbuka kupitia binti yao

"Alilea mwanamume mwenye moyo mwema, na huo ndio urithi wake,"Aliandika Karen.

Muhtasari
  • Nyamu amsifia marehemu mamake Samidoh, asema watamkumbuka kupitia binti yao
Nyamu asema anataka mtoto mwingine
Nyamu asema anataka mtoto mwingine
Image: Instagram

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh amemkumbuka marehemu mama yake ambaye alifariki miaka mingi iliyopita.

Katika chapisho lake  mwanamuziki huyo mahiri ambaye anashabikiwa sana hasa  katika eneo la Mlima Kenya alidokeza kuwa mzazi huyo wake marehemu Miriam Wairimu ndiye msukumo wake mkuu maishani.

"Popote ulipo, popote nitakapokwenda utabaki kuwa chanzo changu cha msukumo," alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Baby mama wake Karen Nyamu alimsifia akisema mama huyo alilea mwanamume mwenye moyo mwema na huo ndio urithi wake.

Aliendelea na kutamani kwamba mabinti walioitwa kwa jina lake wafanane tu naye.

"Alilea mwanamume mwenye moyo mwema, na huo ndio urithi wake,"Aliandika Karen.