Mchungaji apakia ushahidi wa kutabiri kifo cha mwanawe Davido mwezi Januari

Mchungaji huyo mnamo Januari 7 aliandika kwenye Facebook yake kuwa kuna kitu kingetokea katika familia ya Davido na haswa kwa mtoto wake wa kiume.

Muhtasari

• Mwana wa Davido amekufa, akitimiza unabii uliotolewa mnamo tarehe 7 JANUARI 2022 na NABII, - mchungaji huyo alisema.

Image: INSTAGRAM// DAVIDO

Jumanne kulizagaa taarifa za tanzia kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha mtoto wa msanii kutoka Nigeria, Davido.

Iliarifiwa kwamba mtoto huyo alifariki baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogela na kufikia jioni tayari zaidi ya watu 8 walikuwa wameshatiwa nguvuni na vyombo vya dola kwa ajili ya kufanyiwa usaili.

Watu maarufu mbali mbali walijumuika na msanii huyo kuomboleza kifo cha mtoto wake wa kiume huku mitandao ikijaa uvumi na maneno mengine ya kustaajabisha.

Mchungaji mmoja kutoka nchini humo aliweka wazi kwamba kifo cha mtoto wa msanii huyo ni moja ya mambo ambayo aliyatabiri mapema mwaka huu.

Kulingana na mchungaji huyo kwa jina nabii Samwel King, mnamo Januari tarehe 7 mwaka huu alitabiri kifo cha mtoto wa msanii Davido ila akapuuziliwa mbali alipotaka kukutana na familia yake ili kuwataarifu kuhusu utabiri huo.

Alisema kwamba huo ni mwanzo tu kwani atazidi kutoa ufunuo zaidi kuhusu utabiri huo alioutaja kama uliotimia na kuonya watu dhidi ya kupuuza utabiri unaotokana na manabii wa Mungu.

“MUOMBEE DAUDI ADELEKE aka Davido . Katika maono niliona 2022 na fursa nyingi kwake, tuzo na tuzo! Huu ni mwaka mkubwa kwake hata hadi 2023! Lakini tuombe Dhidi ya mshale wowote wa mauti HASA dhidi ya mwanawe! Wapendwa wowote wa karibu. Mungu alinifunulia hili kwamba itatokea ikiwa maombi hayatafanywa. Ninaona T na Y kama kidokezo muhimu sana kwa unabii huu pia. MAMBO YANATOKEA!” Utabiri huo wa mwezi Januari ulisoma.

“UNABII SAHIHI WA ULIMWENGU UMETHIBITISHWA| 🌏 🔥Mwana wa Davido amekufa, akitimiza unabii uliotolewa mnamo tarehe 7 JANUARI 2022 na NABII, na wito wa onyo la kumwombea mwanawe! Mambo muhimu zaidi bado yatatolewa kuelekea UNABII huu kwani kuna DONDOO zilizofichwa ambazo zinahitaji kuwekwa katika maombi tu na familia ya David Adeleke na familia yake!” mchungaji huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.