Nameless aridhika na watoto 3 ataka kufunga uzazi

Nameless ametangaza kuwa anatafuta daktari wa kufanya upasuaji wa kuzuia uzazi

Muhtasari

โ€ข "Ni vizuri wanaume kuzungumzia jambo hilo ili waweze kuwa na maoni mbalimbali na nia wazi ya kubadili dhana zao kuhusu upangaji uzazi," alisema.

Nameless amsifia bintiye kifungua mimba
Nameless amsifia bintiye kifungua mimba
Image: Instagram

Mwanamuziki Nameless amegeuka gumzo mtandaoni baada ya kudokeza kuwa hataki kuongeza watoto wengine.

Katika ukurasa wake wa Facebook, Nameless alisema kuwa anataka kufanya upasuji wa kuzuia uzazi, wa Vasektomi.

"Wueh ๐Ÿฅต... Ati mumesema mtu anaweza pata wapi vasectomist mzuri๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿฅด...#BabaGalzzzzzzz๐Ÿ˜ด๐Ÿ˜ด๐Ÿ˜ด," Nameless aliandika.

Shabiki yake mmoja alimpongeza kwa kutaka kufanyiwa upasuaji huo.

"Haiaminiki jinsi watu wengine haswa wanaume wana fikira hasi kuhusu upasuaji huu," Kajuju Bits &Pieces alisema.

Nameless alikubaliana naye na kumweleza jinsi dhana fikra za jadi zimezuia watu kufikiria na kukubali mabadiliko.

"Ni vizuri wanaume kuzungumzia suala hili ili waweze kuwa na maoni mbalimbali na nia wazi ya kubadilisha imani yao kwa kile kilicho bora na mageuzi ya kitamaduni ya jamii," mwanamuziki huyo wa kibao cha 'Back It Up' alisema.

Mwingine alimwelekeza na kumuunga mkono katika uamuzi wake.

"Nameless, ingia katika hospitali yoyote ya Marie Stopes. Nina furaha kuwa huna fikira kuwa hili ni jambo au tatizo la mwanamke pekee," Nana Amondi alisema.

"Mtoto wako mdogo lazima anakukosesha usingizi, usijali. Baada ya miezi 3 utakuwa unatamani mtoto tena," Nancy Young alisema.

Nameless na mke wake Wahu walimkaribisha binti yao wa tatu hivi majuzi na wamekuwa wakishinikizwa na wanamitandao kupata mtoto wa kiume.

Wapenzi hao wamepuuzilia mbali maoni hayo na kusema kuwa wameridhika kuwa wazazi wa mabinti watatu.

โ€œMimi kama mimi nimeridhika sana na malaika wangu 3 Mungu amenibariki ๐Ÿค—๐Ÿ’. Moyo wangu umejaa zaidi ๐Ÿ™๐Ÿพโค๏ธ. Vinginevyo usiku mwema Kwa wenye mnalala ๐Ÿค—๐Ÿ˜˜..โ€ Wahu alisema.