Vanessa Mdee na Rotimi wafurahia kutarajia mtoto

Wapenzi hao hao walitangaza kutarajia mtoto wa pili wa kike siku chache zilizopita.

Muhtasari

β€’ Vanessa na Rotimi walikuwa wamevaa nguo zinazofanana za rangi nyeupe, wakitembea huku wote wakitabasamu.

Mwanamuziki Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi wameweka mtandaoni  video ya kuvutia inayoonyesha mimba ya Mdee.

Katika video hiyo waliyopakia Instagram, wachumba hao walikuwa wameshikana mkono kwa mahaba.

Walikuwa wamevaa nguo zinazofanana za rangi nyeupe, wakitembea huku wote wakitabasamu.

Rotimi alikuwa akipapasa na kukumbatia tumbo la Mdee.

Mashabiki wao walizidi kuwapongeza huku wakisema jinsi walivyopendeza.

"Inaitwa bandika bandua πŸ”₯πŸ”₯ safi sana 😍😍," duos_bae alisema.

"Unatuwakilisha vizuri Dyadya ,sifa na utukufu kwa Mola wetu muumba wa ardhi na duniaπŸ‘πŸ‘πŸ‘," ashleygolenheart2 alimwambia Mdee.

"Jinsi Rotimi anavyokuangalia 😍😍😍😍 baraka tele kwa familia yako ❀️❀️❀️," _norie_belle aliandika.

Hivi majuzi, wachumba hao walitangaza kutarajia mtoto wa pili wa kike.

" Tunatarajia mtoto wa pili..πŸ™πŸ½πŸŽŠβœ¨UTUKUFU KWA MUNGU ... ni wa kike πŸ’•," Mdee alisema.

Watakuwa na watoto wawili sasa baada ya mtoto wao wa kiume ambaye walimkaribisha duniani mwaka jana.

Mdee na Rotimi wamekuwa wakichumbiana kwa muda sasa na walibarikiwa na mtoto mmmoja ambaye alifikisha mwaka mmoja Septemba 29, mwaka huu.

Vanessa alimmiminia sifa kochokocho mwanawe huku akimshukuru Mungu kwa kumjalia mtoto wa kiume.

"Mtoto wangu, wewe ni zawadi ya kimungu na ninaheshimiwa kuwa Mama yako. Asante kwa kuwa baraka yetu kuu," aliandika

Miezi michache baada ya kumpata mtoto wa kwanza, Rotimi alisema jinsi anafurahia kuwa mzazi na anaridhia sana kusaidia katika malezi wa mwanawe.