Date ya kwanza Lung'aho alinunua chips tukala ndani ya gari usiku - Jackie Matubia

Muigizaji huyo alikuwa akitetea kauli yake kuwa wanaume wa Kenya hawajui kuwahendo wapenzi wao kimapenzi.

Muhtasari

• Siku yetu ya kwanza tulikwenda Chicken Inn, tukapata chakula na kwenda ndani ya gari na kula tu tukiwa tumetulia - Matubia.

Wachumba Blessing Lungaho na Jackie Matubia
Wachumba Blessing Lungaho na Jackie Matubia
Image: Instagram//Maktaba

Kwa muda mrefu kumekuwa na dhana kuwa wengi wa wanaume wakenya hawajui kuwahendo wapenzi wao kwa mapenzi kama yale yanayoigizwa kwenye filamu za Kifilipino na Mexico.

Haya, Mwigizaji wa zamani wa Zora Jackie Matubia amezua kumbukumbu jinsi ambavyo mpenzi wake Blessing Lungaho alivyomuonesha mapenzi katika ‘date’ yao ya kwanza.

Mama huyo wa watoto wawili, kupitia ukurasa wake wa YouTube, alieleza kuwa wanaume Wakenya hawajui kupetipeti wapenzi wao kwa maapenzi na kwamba wengi hushindwa kuwafurahisha wanawake wao kwa kukosa kujifunza lugha zao za mapenzi.

"Wanaume wa Kenya nawapa alama sifuri katika kuonesha mapenzi, kwao na mapenzi nje ya dirisha. Sio ya kimapenzi au aina ya uchumba ya kila siku, lakini ndivyo tulivyokuwa tukifanya na Blessing Lungaho. Siku yetu ya kwanza tulikwenda Chicken Inn, tukapata chakula na kwenda ndani ya gari na kula tu tukiwa tumetulia, ilikuwa karibia saa saba usiku,” Matubia alisema.

Muigizaji huyo alisema kuwa kilichomchukiza si aina ya chakula Lungaho alichokinunua bali ni pale walipoenda kukila na hata aina ya mazungumzo ambayo alikuwa anamhusisha muda wote.

Kulingana na yeye, ni vizuri kuwa na mtu ambaye mnaendana kimazungumzo kuliko kupewa zawadi nzuri na mtu ambaye hakufanyi ujihisi kupendwa kupitia maneno yake mkiwa pamoja.

“Wanaume hapa huvunja benki, na hata hatujali, kwetu ni mazungumzo tu, lakini watu tofauti wana lugha tofauti za upendo.”