Ukimpenda mtu, mheshimu, ikikosekana mapenzi husuasua - Wema Sepetu

Hivi karibuni Sepetu alidokeza kuwa uhusiano wake na Whozu hautadumu hadi kwenye ndoa.

Muhtasari

Kama humpi mwenzako heshima then mapenzi yanakuwa ya kusuasua - Sepetu.

Sepetu ashauri kuhususuhusiano
Sepetu ashauri kuhususuhusiano
Image: Instagram

Mwanafilamu kutoka Tanzania Wema Sepetu ametumia muda wake na ufuasi alionao mkubwa kwenye Instagram kutoa funzo kwa wafuasi wake kuhusu mapenzi.

Sepetu kupitia instastory yake aliachia maelezo marefu akiwashauri watu jinsi ya kufanya mahusian yafanye kazi pasi na misukosuko mingi ambayo huleta nyufa na kusababisha uhusiano kuporomoka.

Kulingana na Sepetu, heshimu ndio nguzo kuu muhimu na ndio huwa kitu cha kwanza kabla ya mapenzi kuja.

Heshima ni kitu muhimu sana kwenye mapenzi...inaanza heshima alafu ndiyo mapenzi... Ukimpenda mtu muheshimu...!!! Kama humpi mwenzako heshima then mapenzi yanakuwa ya kusuasua... Waheshimuni muwapendao,” Wema Sepetu alishauri.

Ni wiki chache tu zilizopita ambapo mwanafilamu huyo alidokeza kuwa huenda uhusiano wake wa kimapenzi na mwanamuziki Whozu hautadumu na wala haoni kama watamalizia katika ndoa.

Mimi sijui, naona kidogo ndoa… ndoa yaani siko tayari kuolewa na Whozu,” Sepetu alisema kwa kudokeza huku klipu hiyo ikikatika.

 Itakumbukwa Wema Sepetu na msanii Whozu walianza uhusiano wao takribani mwezi mmoja uliopita na wamekuwa wakipigwa vita mitandaoni ambapo wengi wanasema anajidhalilisha kuingia katika uhusiano na Whozu ambaye wengi walimtaja kama mdogo si tu kiumri bali pia kiumaarufu.

Wiki kadhaa zilizopita, Whozu alimpeleka Sepetu kisiwani Zanzibar kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo walipakia picha za kutmanisha wakijivinjari na kula bata aliyenona.