Mbona mnafanana na Samidoh sasa? - Wanamitandao wamuuliza Karen Nyamu

Hii ni baada ya kupakia picha akiwa Marekani ambapo wengi hawakusita kugundua mfanano wake na Samidoh.

Muhtasari

• “Tabasamu lisikudanganye, hapa ni baridi promax,” Nyamu aliandika.

• “Kwa nini sasa mnafanana?” Mwingine kwa jina Vickie Rushi alimuuliza.

Karen Nyamu na mzazi mwezake Samidoh
Karen Nyamu na mzazi mwezake Samidoh
Image: Instagram

Seneta maalum Karen Nyamu anazidi kuwapa kiwewe na changamoto wapenzi baada ya kumfuata baba wa watoto wake Marekani.

Akiwa huko Marekani, Nyamu amepakia picha yake akiwa amevalia nguo mfanano juu chini na kusema kwamba huko Marekani sasa hivi baridi iko huko ni ya kiwango cha juu kuzidi maelezo.

“Tabasamu lisikudanganye, hapa ni baridi promax,” Nyamu aliandika.

Lakini kama walivyo wambea na wanoko wa mitandaoni, baadhi walimtania kuwa tabasamu lake lilikuwa limefana na la baba watoto wake msanii Samidoh.

“Unafanana na Samidoh sana hapa,” Beth Wambui alimtania na kuvutia wat uwengi kufanyia sura ya Samidoh na Nyamu udadisi wa kijasusi.

“Kwa nini sasa mnafanana?” Mwingine kwa jina Vickie Rushi alimuuliza.

“Watu wakipenda wananzanza kufanana na ukweli ni utabaki kuwa Samidoh anapenda Karen kuliko mkewe,” Gathuru alisema.

Nyamu na Samidoh wana watoto wawili licha ya kujua fika kuwa msanii huyo ambaye pia ni afisa wa polisi ana mke wa kwanza na kuwa na watoto pia naye.

Hivi karibuni, Nyamu alimkaripia mtumizi wa mitandao aliyemwambia kwamba Samidoh hampendi na ndio maana hajawahi kupakia picha zake kwenye mitandao ya kijamii lakini Nyamu akamwambia kwamba si lazima apakiwe ndio ajue anapendwa.

Alizidi kusema kuwa mkewe Samidoh anahitaji heshima yake na kupakia picha zake ni jambo ambalo litakuwa si la kuonesha heshima kwa mke wa kwanza, Edday Nderitu.