Thamani ya Samidoh inastahili kupiganiwa- Karen Nyamu

"Simpiganii, lakini anastahili kupiganiwa," alijibu.

Muhtasari

•Karen alikuwa akijibu mojawapo ya maswali aliyoulizwa katika kipindi cha maswalina majibu ambacho aliwashirikisha watumizi wa Instagram alipokuwa kwenye safari ya kuelekea Congo.

•Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanasiasa huyo kudaiwa kuzozana na mwanadada mwingine juu ya Samidoh.

Samidoh na Karen Nyamu
Samidoh na Karen Nyamu
Image: INSTAGRAM

Wakili na Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu ameweka wazi kuwa hampiganii baba wa watoto wake wawili, Samidoh.

Mama huyo wa watoto watatu alikuwa akijibu mojawapo ya maswali aliyoulizwa katika kipindi cha maswali na majibu ambacho aliwashirikisha watumizi wa Instagram alipokuwa kwenye safari ya kuelekea Congo.

"Je, unampigania Samidoh?" shabiki aliuliza.

Katika jibu lake, Bi Nyamu alibainisha kuwa staa huyo wa nyimbo za Mugithi anastahili kupiganiwa. 

"Simpiganii, lakini anastahili kupiganiwa," alijibu.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanasiasa huyo kudaiwa kuzozana na mwanadada mwingine juu ya Samidoh.

Wanamitanadao walikuwa wakimtaja Karen kwenye posti za promota wa Samidoh, Bernice akitoa taarifa kuhusu shoo zake. Baadhi walikuwa wakimshauri akae macho wakidai kwamba Berinice alitaka 'kumwiba' Samidoh kutoka kwake.

Kufuatia shinikizo nyingi, hatimaye alijibu.

Shabiki aliyetambulika kama Eunice Shaisha alimwambia Karen azibe masikio yake mradi tu Samidoh alipe bili.

Karen alijibu; "Watu wa Marekani wanajitokeza kwa wingi kumuona Bernice ambaye ana mali kubwa na pia kufurahia Mugiithi. Pia, wanapiga picha na kuitumia."

Katika chapisho lingine kwenye ukurasa wake wa Instagram, Karen alipakia video ya mwanamke akipiga mbizi majini na kusema hivyo ndivyo watu wanavyojilazimisha katika mahusiano ya watu wengine.

Katika ukurasa wake rasmi wa Facebook, Bernice alijibu akisema hatamjibu baby mama huyo wa Samidoh.

"Ninakaa na kuwatazama wakitukana, ndivyo nilivyolelewa mimi sio muoga bali nina busara." alisema.

Pia alinukuu biblia akisema kuwa heri wafanya amani maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Aliongeza kwamba Biblia haisemi kwamba wale wenye furaha lazima wawe sahihi wakati wote bila kujali ni inagharimu nini.

Hatimaye aliwataka Wanamtandao kuwa walinda amani.